George Kavishe |
MBIO za
Kilimanjaro Marathon mwaka huu zinatajiwa kuwa na washiriki wa kigeni wapatao
600 kutoka nchi zaidi ya 40.
John
Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema
katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kuwa mbio hizo zinaendelea
kuwavutia washiriki wengi wa kimataifa kutokana na jitihada za pamoja
zinazofanywa na waandaaji pamoja na bia ya Kilimanjaro Premium Lager katika
kutangaza tukio hili. Hii ndi sababu iliyochangia ukuaji wa mbio hizi pamoja na
ushiriki kuongezeka kila mwaka.
Addison
alisema washiriki wengi zaidi watatoka Marekani ikifuatiwa na Uingereza. Nchi
nyingine zinazotarajiwa kushiriki ni pamoja na Canada, Japan, Uganda, Zimbabwe
na Kenya. Nyingine ni pamoja na Sweden, Australia, Hungary, Germany, Zambia, Morocco, Swaziland, Nigeria na
Malawi.
Zikiwa
zimepangwa kufanyika Moshi tarehe 3 Machi 2013, mbio za Kilimanjaro Marathon
zitakuwa zimegawanyika katika sehemu nne ambazo ni 42km Kilimanjaro Premium
Lager Marathon, 21km Half Marathon, GAPCO
Disabled Half Marathon na Vodacom 5km Fun Run.
Mbio hizo
pia zinatarajiwa kuchangamshwa na ushiriki wa timu za makampuni ambapo
wafanyakazi wa makampuni wadhamini watashindana katika mbio ya nusu marathon
kupitia shindano litakalojulikana kama“Half Marathon Corporate Challenge”.
Makampuni ambayo yameishathibitisha kushiriki shindano hilo ni pamoja na TPC
Sugar ambao ndio mabingwa watetezi wa shindano hilo wakifuatiwa na CFAO Motors,
TanzaniteOne na Tanga Cement.
Addison
alisema kuwa mbio za Kilimanjaro Marathon zinaingia katika mwaka wa 11 tangu
kuanzishwa zikiwa zimesajiriwa rasmi na shikisho la riadha la kimataifa na
kuongeza kuwa kutakuwepo na vituo vya maji pamoja na viburudisho katika njia ya
mashindano hayo.
“Mbio hii
inafanyika chini ya Mlima Kilimanjaro ambapo kila mtu anaweza kukimbia kwa raka
kwani urefu wake kutoka usawa wa bahari ni wastani wa mita 830 mpaka 1150
katika barabara nzuri yenye lami. Inatarajiwa kuwa shamrashamra maana wananchi
wengi watajitokeza pembezoni mwa
barabara kuwashangilia na kuwapa moyo wakimbiaji, na wakimbiaji wa
kujifurahisha wanaweza hata kusimama kupata kiburudisho njiani”, Addison
aliitimisha.
Mbio hizo
zinadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager (wadhamini wakuu), Vodacom Tanzania
(5km Fun Run), GAPCO (Disabled Half Marathon), Tanga Cement, CFAO Motors, KK
Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, New Arusha Hotel na Kilimanjaro
Water.
No comments:
Post a Comment