Sunday, January 13, 2013

TIMU YA RHINO RANGERS YAIVUNJA VUNJA TIMU ILIYOCHAGULIWA KUUNDA KOMBAINI WILAYA


 

 Timu ya wanajeshi ya mkoani Tabora ambayo inajiandaa na ligi daraja la kwanza imewatandika bila huruma kombaini ya wilaya mkoani Tabora mabao 2-0 katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu kuelekea katika mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza FDL ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi tarehe 26/1/2013.

Mabao ya Rhino rangers yalifungwa na shija sanju dk ya 33 na mchembe dk ya 44  kipindi cha kwanza  baada ya mabeki wa kombain wilaya kujichanganya na kuwaruhusu rhino kujipatia mabao hayo mawili yaliyowawezesha kutoka uwanjani kifua mbele kwa mabao 2-0.

 Timu hiyo ya rhino inaendelea na mazoezi yake tena kesho jumatatu katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi wakiwapashia nguvu wakata miwa wa bukoba  KAGERA SUGAR ambao wanatarajia kuja kucheza nao tarehe 18/1/2013 pia wanatarjia kucheza na timu ya Azam Fc na timu ya Simba B katika uwanja wa A.H. MWINYI ili kujua ni jinsi gani wanamapungufu yao.

Naye mwenyekiti wa TAREFA mkoa wa tabora bw. YUSUPH KHAMIS KITUMBO amewahakikishia timu ya RHINO RANGERS pamoja na polisi kuwa wajiandae kwani anafanya mawasiliano ili waje kuwapa nguvu kazi ya mzunguko wa pili wa daraja la kwanza FDL.

WACHEZAJI WA RHINO RANGERS WAKIWA WAMEPOOZI BAADA YA HLF TIME WAKIWA MBELE KWA BAO 2-0

WACHEZAJI WA TIMU YA KOMBAINI WILAYA  MKOA WA TABORA WAKIWA HOI BAADA YA KUPIGISHWA KWATA NA WANAJESHI KIPINDI CHA KWANZA 2-0
 
KOCHA MSAIDIZI NA MCHEZAJI WA ZAMANI WA MILAMBO DIDAS KUNDE  AKIWAPA SOMO WACHEZAJI WAKE PEMBENI NI KOCHA MKUU ANDREW ZOMA

No comments:

Post a Comment