Sunday, January 13, 2013

AFCON 2013: MFALME wa MAGOLI AFRIKA, NANI KUTWAA TAJI??

>>AFCON 2012 WACHEZAJI 7 WALIFUNGANA UFUNGAJI BORA!!
AFCON_2013_LOGO>>UNAMJUA WILFRIED BONY, MWAFRIKA PEKEE ANAEONGOZA ULAYA KWA UFUNGAJI LIGI KUBWA??
AFCON 2013, Kombe la Mataifa ya Afrika, linaanza huko Afrika Kusini Januari 19 na ikifika Februari 10 Bingwa wa Afrika atapatikana miongoni mwa Nchi 16 ambazo zipo kwenye Fainali lakini pia kinyang’anyiro kingine ni ule ushindani wa Wachezaji Masupastaa kutaka kuibuka kama Mfungaji Bora, kitimtim ambacho ni kigumu hasa ukizinagatia katika Mashindano yaliyopita, AFCON 2012, yaliyochezwa Nchini Equatorial Guinea na Gabon  Mwezi Januari 2012, Wachezaji 7 walifungana kwa kupiga Bao 3 kila mmoja.
Saba hao wa AFCON 2012 ni Manucho (Angola), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon), Didier Drogba (Ivory Coast), Cheick Tidiane Diabate (Mali), Houcine Kharja (Morocco) Chris Katongo na Emmanuel Mayuka (Wote Zambia).
Kati ya hao 7, Drogba, Wazambia Chris Katongo na Emmanuel Mayuka, Cheick Tidiane Diabate wa Mali na Manucho wa Angola watakuwepo AFCON 2013.
Lakini, Samuel Eto’o wa Cameroun, Mchezaji ambae ndie anashikilia Rekodi ya kufunga Bao nyingi kwenye AFCON, Bao 18 katika Fainali 6, hayupo kwenye Mashindano haya kwa vile Cameroun, kwa mara nyingine tena, haimo kwenye AFCON 2013.
Mbali ya Majina yaliyozoeleka kama kina Didier Drogba, ipo ‘Mashine mpya ya Magoli’ ya Ivory Coast, Wilfried Bony, ambae anachezea Klabu ya huko Holland, Vitesse Arnhem, na tayari kwenye Ligi Nchini humo ashapiga Bao 16 katika Mechi 18 na kumfanya awe ndie aneongoza kwa Magoli kwenye Ligi hiyo, akiwa ni Mchezaji pekee toka Barani Afrika ambae anaongoza kwa Ufungaji katika Ligi kubwa huko Ulaya.
Wengine toka Afrika wanaotamba kwa Ufungaji Mabao na watakuwepo kwenye AFCON 2013 ni Lancina Traore ambae ameshaifungia Anzhi Makhachkala kwenye Ligi ya Urusi Bao 9 ikiwa ni Bao moja zaidi ya Ahmed Mussa wa CSKA Moscow ambae yupo na Timu ya Taifa ya Nigeria huko Afrika Kusini.
Manucho, ambae aliwahi kuichezea Manchester United, anazo Bao 6 kwa Klabu yake ya Spain, Real Valladolid, zikiwamo Bao 2 alizoipiga Real Madrid walipokutana Mwezi uliopita.
Mchezaji wa Togo anaecheza Tottenham Hotspur, Emmanuel Adebayor, Siku zote amekuwa akifunikwa na kina Didier Drogba na Samuel Eto’o lakini pengine safari hii ni muda wake.
WAFUNGAJI BORA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA:
-1957 (Sudan) - Ad El Diba (Egypt) MABAO 5
-1959 (Egypt) - Mahmoud Al Gohari (Egypt) 3
-1962 (Ethiopia) - Mohamed Al Badawi (Egypt), Worku Mengistu (Ethiopia) 3
-1963 (Ghana) - Ahmed Al Chazli (Egypt) 6
-1965 (Tunisia) - Abbrey Osei Kofi (Ghana), Eustace Mangli (Ivory Coast) 3
-1968 (Ethiopia) - Laurent Pokou (Ivory Coast) 6
-1970 (Sudan) - Laurent Pokou (Ivory Coast) 8
-1972 (Cameroon) - Salif Keita (Mali), 5
-1974 (Egypt) - Mulamba Ndaye (Zaire) 9
-1976 (Ethiopia) - William Njo Lea (Guinea) 4
-1978 (Ghana) - Phillip Omondi (Uganda) 4
-1980 (Nigeria) - Segun Odegbami (Nigeria) 3
-1982 (Libya) - George Al Hassan (Ghana) 4
-1984 (Ivory Coast) - Taher Abou Zeid (Egypt) 4
-1986 (Egypt) - Roger Milla (Cameroon), Abdoulaye Traore (Ivory Coast) 4
-1988 (Morocco) - Lakhdar Belloumi (Algeria), Roger Milla (Cameroon), Gamal Abdelhamid (Egypt), Abdoulaye Traore (Ivory Coast) 4
-1990 (Algeria) - Djamel Menad (Algeria) 4
-1992 (Senegal) - Rachidi Yekini (Nigeria) 4
-1994 (Tunisia) - Rachidi Yekini (Nigeria) 5
-1996 (South Africa) - Kalusha Bwalya (Zambia) 5
-1998 (Burkina Faso) - Hossam Hassan (Egypt), Benni McCarthy (South Africa) 7
-2000 (Ghana and Nigeria) - Shaun Bartlett (South Africa) 5
-2002 (Mali) - Patrick Mboma, Salomon Olembe (both Cameroon), Julius Aghahowa (Nigeria) 3
-2004 (Tunisia) - Patrick Mboma (Cameroon), Frederic Kanoute (Mali), Austin Okocha (Nigeria), Youssef Mokhtari (Morocco), Francileudo dos Santos (Tunisia) 4
-2006 (Egypt) - Samuel Eto'o (Cameroon), Ahmed Hassan (Egypt) and Francileudo dos Santos (Tunisia) 4
-2008 (Ghana) - Samuel Eto'o (Cameroon) 5
2010 (Angola) - Mohamed Nagui (Egypt) 5
2012 (Equatorial Guinea and Gabon) - Manucho (Angola), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon), Didier Drogba (Ivory Coast), Cheick Tidiane Diabate (Mali), Houcine Kharja (Morocco) Chris Katongo, Emmanuel Mayuka (Wote Zambia) 3.

No comments:

Post a Comment