Sunday, January 13, 2013

MANCHESTER UNITED WAIADABISHA LIVERPOOL OTRAFORD NA KUWARUDISHA KATIKA JIJI LA MERCYSIDE VICHWA CHINI

>>UNITED WAKO POINTI 10 MBELE, KILELENI!
BPL_LOGOManchester United leo wamezidi kupaa kileleni baada ya kuwachapa Mahasimu wao wakubwa Liverpool Bao 2-1 Uwanjani Old Trafford na kukwea juu kileleni mwa BPL, Barclays Premier League, wakiwa Pointi 10 mbele ya Timu ya Pili Man City ambao muda mfupi baadae leo wana kibarua kigumu Uwanjani Emirates watakapoivaa Arsenal.RVP-BAO_NA_LIVERPOOL
++++++++++++++++
MAGOLI:
Man United 2
-Van Persie Dakika ya 19
-Vidic 54
Liverpool 1
-Sturridge Dakika ya 57
++++++++++++++++
Man United, ambao walitawala kabisa Kipindi cha Kwanza, walifunga Bao lao la kwanza kupitia Robin van Persie kufuatia pasi murua kati ya Danny Welbeck, Tom Cleverley, Shinji Kagawa na Patrice Evra kumtilia pasi ya chini Van Persie aliepachika wavuni kiakili.
Frikiki ya Robin van Persie iliunganishwa kwa kichwa na Patrice Evra na kumparaza Nemanja Vidic na kutinga wavuni na kuwapa Man United Bao la Pili.
Lakini, Dakika chache baadae, makosa ya Man United yaliwapa Liverpool Bao laini baada ya shuti la Steven Gerrard kutemwa na Kipa David De Gea na kutua njiani kwa Mchezaji mpya Daniel Sturridge alieunganisha vizuri na kufunga Bao lake la kwanza kwenye BPL kwa Timu yake mpya na Bao lake la pili baada ya pia kuifungia kwenye FA CUP walipoichapa Mansfield 2-1 kwenye Mechi yake ya kwanza kabisa hivi majuzi.
VIKOSI:
Manchester United: De Gea, Da Silva, Ferdinand, Vidic, Evra, Carrick, Cleverley, Young, Kagawa, Welbeck, van Persie
Akiba: Amos, Jones, Valencia, Anderson, Giggs, Smalling, Hernandez.
Liverpool: Reina, Wisdom, Skrtel, Agger, Johnson, Lucas, Downing, Gerrard, Allen, Sterling, Suarez
Akiba: Jones, Henderson, Sturridge, Carragher, Borini, Shelvey, Robinson.
Refa: Howard Webb
+++++++++++++++++++++++
BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA:
Jumapili 13 Januari 2013
[SAA 1 Usiku]
Arsenal v Man City
Jumatano Januari 16
[SAA 4 DAK 45 Usiku]
Chelsea v Southampton
Jumamosi Januari 19
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Norwich
Man City v Fulham
Newcastle v Reading
Swansea v Stoke
West Ham v QPR
Wigan v Sunderland
[SAA 2 na Nusu Usiku]
West Brom v Aston Villa
Jumapili Januari 20
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Chelsea v Arsenal
[SAA 1 Usiku]
Tottenham v Man United

No comments:

Post a Comment