Sunday, January 13, 2013

BPL: LEO ni MAN UNITED v LIVERPOOL & ARSENAL v MAN CITY!!!


BPL_LOGOZIFUATAZO NI DONDOO MUHIMU KUHUSU BIGI MECHI ZA LEO:
MANCHESTER UNITED v LIVERPOOL
-UWANJA: Old Trafford
-TAREHE: Jumapili, 13 Januari
HALI za WACHEZAJI
Nani na Anderson wamepona maumivu yao na wamerejea kwenye Kikosi na huenda leo wakapata nafasi ya kucheza kwa wakati fulani.
Nae Wayne Rooney amepona tatizo la Goti lakini Mechi hii imedaiwa ni mapema kwake na atacheza Mechi ya marudiano ya FA Cup dhidi ya West Ham hapo Jumatano.
Liverpool watawakosa Jose Enrique na Martin Kelly na hilo litawalazimu kumchezesha Andre Wisdom kama Fulbeki wa kulia na Glen Johnson kucheza kama Fulbeki wa kushoto.
Mchezaji mpya wa Liverpool Daniel Sturridge, alienunuliwa kutoka Chelsea, leo anaweza kuanza Mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu England baada ya kucheza na kufunga Bao kwenye FA CUP Wiki iliyopita Liverpool walipoifunga Mansfield Bao 2-1.
USO kwa USO 
-Manchester United wameshinda Mechi 7 kati ya 8 za Ligi zilizochezwa mwishoni Uwanjani Old Trafford na ushindi pekee wa Liverpool ni ule wa Machi 2009 waliposhinda 4-1.
VIKOSI:
Manchester United (Mfumo: 4-3-1-2): De Gea; Rafael, Ferdinand, Evans, Evra; Valencia, Carrick, Cleverley; Kagawa; Hernandez, Van Persie.
Liverpool (Mfumo: 4-3-3): Reina; Wisdom, Skrtel, Agger. Johnson; Lucas, Gerrard, Downing; Sterling, Suárez, Sturridge.
Refa: Howard Webb (Mechi 16, Kadi Nyekundu 2, Kadi za Njano 57).
ARSENAL v MANCHESTER CITY
-UWANJA: Emirates Stadium
-TAREHE: Jumapili, 13 Januari
HALI za WACHEZAJI
Arsenal huenda wakamkosa Olivier Giroud ambae alichanika Goti walipotoka sare na Swansea katika Mechi yao ya mwisho.
Baada ya kuwa nje kwa Miezi mitatu akijiuguza Paja, Kiungo Abou Diaby huenda akapata Namba baada Juzi kurejea Uwanjani kwa kuichezea Timu ya Vijana ya Arsenal ya chini ya Miaka 21.
Manchester City itawakosa Sergio Aguero, tatizo la Goti,  Samir Nasri, Kifungoni, na Ndugu wawili, Yaya na Kolo Toure, ambao wako na Timu yao ya Taifa ya Ivory Coast kwa ajili ya AFCON 2013.
USO kwa USO 
-Manchester City wameshacheza Mechi 27 za Ligi bila kushinda nyumbani kwa Arsenal. Ushindi wao wa mwisho ulikuwa Uwanja wa Highbury katika ile Ligi ya zamani ya Daraja la 1 Mwaka 1975.
-Manchester City hawajafunga hata Bao moja katika mara 5 za mwisho walizotua kwenye Uwanja wa Arsenal. Mchezaji wao wa mwisho kufunga Bao alikuwa ni DaMarcus Beasley, aliefunga Bao lao pekee walipochapwa 3-1 Aprili 2007.
VIKOSI:
Arsenal (Mfumo: 4-2-3-1): Szczesny; Sagna, Mertesacker, Vermaelen, Gibbs; Arteta, Wilshere; Oxlade-Chamberlain, Cazorla, Podolski; Walcott.
Manchester City (Mfumo: 4-2-3-1): Hart; Zabaleta, Kompany, Nastasic, Clichy; Garcia, Barry; Silva, Tévez, Milner; Dzeko.
Refa: Mike Dean (Mechi 14, Kadi Nyekundu 1, Kadi za Njano 49).

No comments:

Post a Comment