Sunday, January 13, 2013

HALI NDANI YA REAL MADRID YAZIDI KUYEYUKA LA LIGA: REAL MAJI SHINGONI YABANWA NA VIBONDE 0-0 HIYO JANA

>>YASHINDWA KUIFUNGA OSASUNA ILIYO MKIANI!!
>>LEO VINARA BARCA DIMBANI!!
BARCA_v_REALJose Mourinho na Timu yake Real Madrid wamezidi kuingia kwenye presha kubwa ya kusakamwa na Mashabiki baada ya jana kushindwa kuifunga Osasuna ambayo ni moja ya Timu 3 zilizo mkiani baada ya kutoka sare 0-0 katika Mechi ya La Liga iliyozidi kuwathibitishia kuwa Msimu huu Ubingwa umewatoka.
Usiku wa jana ulikuwa wa balaa kwa Real Madrid ambao walicheza bila Nyota wao, Cristiano Ronaldo na Sergio Ramos, ambao wanatumikia Kifungo, nae Mchezaji wao Kaka, alieanzia Benchi, alidumu Dakika 19 tu Uwanjani na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada ya kupata Kadi za Njano mbili na Bao lao safi lililofungwa na Jose Maria Callejon kukataliwa kwa Ofsaidi ya utata.
Matokeo hayo yamewafanya Real Madrid wawe Pointi 4 nyuma ya Atletico Madrid, walio nafasi ya pili, na Pointi 15 nyuma ya Vinara Barcelona.
Barcelona na Atletico Madrid wanaweza kuzidisha mapengo yao hayo hivi leo baada ya Mechi zao.
HUKO Italy, jana kulikuwa na Mechi mbili za Serie A kwa Bologna kuipiga Chievo Verona 4-0 na Inter Milan kuifunga Pescara 2-0.
RATIBA/MATOKEO:
LA LIGA
Jumamosi Januari 12
Real Valladolid 3 Real Mallorca 1
RCD Espanyol 1 Celta de Vigo 0
Osasuna 0 Real Madrid 0
Valencia 2 Sevilla FC 0
Jumapili Januari 13
Real Betis v Levante
Real Sociedad v Deportivo La Coruna
Atletico de Madrid v Real Zaragoza
Malaga CF v FC Barcelona
Jumatatu Januari 14
Getafe CF v Granada CF
SERIE A
Jumamosi Januari 12
Bologna 4 Chievo Verona 0
Inter Milan 2 Pescara 0
Jumapili Januari 13
Torino FC v Siena
SS Lazio v Atalanta
Parma v Juventus
Udinese v Fiorentina
Napoli v Palermo
Cagliari v Genoa
Catania v AS Roma
Sampdoria v AC Milan

No comments:

Post a Comment