Saturday, January 5, 2013

ANDY MURRAY KUTWAA UBINGWA BRISBANE INTERNATIONAL KESHO?



BRISBANE, Australia
NYOTA wa tenisi raia wa Uingereza, Andy Murray, 25, kesho Jumapili anakutana uso kwa uso na Grigor Dimitrov wa Ubelgiji katika fainali ya michuano ya Brisbane International, huku akipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa mashindano hayo.
Murray alitinga kirahisi fainali ya michuano hiyo baada ya mpinzani wake katika mechi ya nusu fainali, Kei Nishikori kujitoa mchezoni kutokana na kuumia goti.
Murray anayeshikilia nafasi ya tatu kidunia kwa ubora wa tenisi na namba moja kwa Uingereza, alirudi vema kutoka mapumziko na kutoka nyuma na kushinda 6-4 katika mechi za seti tatno mfululizo.
Mkali huyo alikuwa mbele kwa seti 2-0 katika nusu ya pili ya pambano lao, wakati Nishikori wa Japan alipoamua kujitoa rasmi na kumruhusu Mskochi huyo kutinga fainali.
Kesho Murray ataoneshana ubabe na mkali wa mchezo huo Dimitrov raia wa Ubelgiji, ambaye alimshinda Marcos Baghdatis wa Cyprus kwa 6-3 5-7 7-6 (7-5) katika nusu fainali nyingine ya michuano hiyo.
Brisbane International ni michuano inayochukuliwa kama sehemu ya maandalizi ya Murray, anayejiweka tayari kwa mashindano ya Australian Open, yatakayofanyika kwa wiki mbili kuanzia Januri 14 hadi 27, jijini Melbourne.

No comments:

Post a Comment