Saturday, January 5, 2013

PRINCE-BOATENG ALIFANYA MAKOSA - SEEDORF.


MCHEZAJI nguli wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya AC Milan Clerence Seedorf amesema Kevin-Prince Boateng ambaye alikuwa mchezaji mwenzake katika klabu alifanya vibaya kuwaongoza wenzake kuondoka uwanjani kwasababu ya kufanyiwa vitendo vya kibaguzi. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ghana alikamata mpira kisha kuupiga kwa mashabiki ambao walikuwa wakishangilia kwa kutoa kelele za nyani kwa wachezaji weusi wa Milan na kusababisha mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Pro Patria uliochezwa Alhamisi kuvunjika dakika ya 25. Pamoja na Seedorf kuponda tukio hilo lakini Patrick Vieira, Rio Ferdinand na Vincent Kompany waliunga mkono kwa nyakati tofauti kitendo kilichofanywa na Prince Boateng. Seedorf ambaye kwasasa anacheza katika klabu ya Botafogo ya Brazil alitegemea tukio tofauti na hilo ili kupambana na mashabiki hao wabaguzi badala kuondoka uwanjani na kususia mchezo. Nyota huyo amesema ingekuwa vizuri zaidi kama Boateng angewatambua mashabiki hao wabaguzi na kisha kuamriwa kutoka nje ya uwanja na mchezo uweze kuendelea na sio kususia mchezo kwani unawanyima burudani mashabiki wengi wastaarabu ambao walikuja uwanja kutizama mechi. Seedorf amecheza Milan kuanzia mwaka 2002 mpaka 2012 na kufanikiwa kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya m waka 2003 na 2007.

No comments:

Post a Comment