Saturday, January 5, 2013

BLATTER AGUSWA NA VIFO VILIVYOTOKEA NCHINI IVORY COAST.


RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter ametuma barua ya salamu rambirambi kwa Shirikisho la Soka nchini Ivory Coast na nchi nzima kwa ujumla kufuatia vifo vya watu 61 vilivyotokea katika mkesha wa mwaka mpya jijini Abidjan. Katika barua hiyo Blatter ameeleza kusikitishwa kwake na taarifa hizo za kuhuzunisha za vifo hivyo ambavyo vilitokea baada ya kukanyagana wakati watu wakikimbia kuangalia mafataki kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya 2013. Amesema kwa niaba ya FIFA nay eye mwenyewe anapenda kutuma salamu zake za rambirambi kwa shirikisho hilo, familia za wahanga wa tukio hilo pamoja na watu wote wa Ivory Coast. Wahanga wengi katika tukio hilo walikuwa ni watu wenye umri kati ya miaka 8 mpaka 18 ambapo rais wan chi hiyo alitangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Jumatano iliyopita.

No comments:

Post a Comment