Saturday, January 5, 2013

BA RASMI CHELSEA, COLE RASMI WEST HAM, BALOTELLI ‘NAFASI 100!’

>>CHAMAKH NAE ATU WEST HAM KWA MKOPO!!
>>LIVERPOOL YAMLIPA COLE PAUNI MILIONI 3 KUNG’OKA!
DEMBA_BA-AENDA_CHELSEAUHAMISHO umepamba moto huku Demba Ba akithibitishwa kuihama Newcastle na kutua Chelsea, West Ham ikiwapata Joe Cole kutoka Liverpool na kumchukua Straika wa Arsenal Marouane Chamakh kwa mkopo lakini Mario Balotelli atabaki Manchester City baada ya Meneja Roberto Mancini kutamka atampa ‘nafasi 100’ ili ajirekebisha baada ya jana kutaka kutwangana nae mazoezini.
DEMBA BA
Chelsea imemsaini Demba Ba, Miaka 27, kutoka Newcastle kwa Mkataba wa Miaka mitatu na nusu na kwa Dau ambalo halikutajwa.


REKODI YA DEMBA BA:
-Alizaliwa Paris, France ikiwa ni mmoja wa Watoto wanane
-Klabu alizowahi kuchezea: Rouen, Mouscron, Hoffenheim, West Ham, Newcastle
-Aliifungua West Ham Bao 7 katika Mechi 12 alizocheza za Ligi Kuu England
-Alifunga Bao 17 katika Msimu wake wa kwanza na Newcastle
-Msimu huu ameshapachika Mabao 13 kwa Newcastle

Ba, ambae alihamia Newcastle kutoka West Ham Mwezi Juni 2011, anambadili Daniel Sturridge alieihama Chelsea kwenda Liverpool hivi juzi.
Demba Ba anaruhusiwa kuichezea Chelsea kwenye Mechi yao ya Jumamosi ya FA CUP dhidi ya Southampton na ile Nusu Fainali ya CAPITAL ONE CUP ambayo watacheza na Swansea lakini haruhusiwi kucheza UEFA EUROPA LIGI kwa vile alishawahi kuichezea Newcastle kwenye Mashindano hayo.


WEST HAM
West Ham imewanasa Joe Cole kutoka Liverpool kwa Uhamisho wa bure bila kulipa chochote na pia Marouane Chamakh ambae atakuwa hapo kwa Mkopo hadi mwishoni mwa Msimu.
Cole, mwenye Miaka 31 ambae alihamia Liverpool kutoka Chelsea Mwaka 2010 pia kwa Uhamisho wa bure, amekuwa hana namba Liverpool na Msimu uliopita alipelekwa kuchezea Klabu ya France Lille kwa Mkopo.
Cole amepewa Mkataba wa Miezi 18 na West Ham, Klabu ambayo alianzia Soka lake, na yupo huru kucheza dhidi ya Manchester United Jumamosi kwenye Mechi ya FA CUP itakayochezwa Upton Park.
+++++++++++++++++++++++++++++++
REKODI ya JOE COLE:
-West Ham: Mechi 150 Magoli (1999-2003)
-Chelsea: Mechi 282 Magoli (2003-2010)
-Liverpool: Mechi 42 Magoli 5 (2010-2013)
-Lille: Mechi 38 Magoli 4 (Mkopo 2011-2012)
-England: Mechi 56 Magoli 10 (2001-2010)
+++++++++++++++++++++++++++++++
Inaaminika Liverpool imekubali kumlipa Joe Cole Pauni Milioni 3 ili ahame ili wao waokoe Pauni Milioni 4 ambazo angelipwa kama angeendelea kubakia Klabuni hapo hadi Mkataba wake unakwisha baada ya Miezi 18 huku akipokea Mshahara wa Pauni 92,000 kwa Wiki.
Huko West Ham atalipwa Pauni 50,000 kwa Wiki.
Wakati huo huo, West Ham imemchukua Straika wa Arsenal Marouane Chamakh kwa Mkopo hadi mwishoni mwa Msimu.
Ingawa Straika huyo amekuwa hana namba ya kudumu huko Arsenal tangu atue hapo kutoka Bordeaux Mwaka 2010, Meneja wa West Ham, Sam Allardyce, amesema amelazimika kupata Straika mwingine kwa vile Andy Carroll ni majeruhi, Modibo Keita atakuwa hayupo kwa vile anaenda kucheza AFCON 2013 na wamebakiwa na Straika mmoja tu, Carlton Cole.
Hata hivyo, Marouane Chamakh, haruhisiwi kucheza dhidi ya Manchester United Jumamosi kwenye Mechi ya FA CUP itakayochezwa Upton Park kwa vile amechelewa kusajiliwa.


BALOTELLI KUPEWA ‘NAFASI 100!’
Bosi wa Manchester City Roberto Mancini amesema atampa Mario Balotelli "nafasi 100 zaidi" ili ajirekebishe baada ya kuvaana na nusura kutwangana jana mazoezini.MANCINI_n_BALOTELLI-MSHIKEMSHIKE
Hata hivyo Mancini amekana kuhusu kupigana na ametamka: "Hamna kupigana, si kweli. Picha zinaonyesha vibaya!”
Akaongeza: “Nitampa nafasi 100 zaidi ikiwa upo uwezekano wa yeye kubadilika. Nampa nafasi nyingine kwa vile ana Miaka 22 na anaweza kufanya makosa!”
Akisisitiza kuwa Picha zilizochapishwa kwenye Vyombo vya Habari zimepotosha ukweli, Mancini alisema: “Haikuwa mbaya kiasi kile! Tulikuwa tunacheza gemu na Mario akampiga teke Mchezaji mwingine! Nikwambia aondoke Uwanjani, aende ndani na yeye akasema hapana, nikamkunja Jezi na kumsukuma! Haikuwa kitu kikubwa!”

No comments:

Post a Comment