Saturday, January 5, 2013

KIBIBI KIZEE CHA TURIN JUVENTUS WAKANA KUMTAKA DROGBA.



 Antonio Conte amekanusha kuwa Juventus iko kwenye mpango wa kumchukua Didier Drogba kuelekea Turin lakini amesema Fernando Llorente yuko katika mipango ya mapendekezo.
Didier Drogba kwasasa anasaka klabu ya kuelekea kutoka katika klabu yake ya sasa Shanghai Shenhua ya dirisha dogo la usajili.
Juve maarufu kama Bianconeri tangu kufunguliwa kwa  dirisha la usajili wa majira ya baridi, imekamilisha usajili wa mchezaji mmoja tu mlinzi Federico Peluso aliyetokea Atalanta lakini pia wakiwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji.
Drogba, amekuwa akihusishwa na Juve katika kipindi cha hivi karibu wakati ambapo Athletic Bilbao ikiweka wazi kuwa mshambuliaji wao Llorente ameanza mazungumzo ya kujiunga na Juventus mara baadya mkataba wake kumalizika.
MANCINI ASEMA KLABU ILIGUSWA NA NA MZOZO WAKE NA BAOTELLI

 
Roberto Mancini amesisitiza kuwa mmiliki wa klabu na mwenyekiti wa klabu ya Manchester United wameonekana kuridhishwa na hatua yake ya kutaka kumrekebisha kumpa nafasi zaidi Mario Balotelli.
Mancini amesema hapingani na hali ya sintofahamu iliyojitokeza wakati wa mzozo wake na Balotelli katika uwanja wa mazoezi ambapo meneja huyo wa City alionekana kwenye picha akimkunja mshambuliaji wake kijezi cha juu cha mazoezi(bips).
Mtaliano huyo amesema mmiliki wa klabu Sheikh Mansour na mwenyekiti wa klabu Khaldoon al Mubarak wamekubaliana na mawazo yake ya kutaka kumpa muda zaidi wa kujirekebisha sambamba kumpa fursa nyingine.
Amenukuliwa Mancini akisema,
"kwakweli wananipa sapoti mimi na timu kwa ujumla na nadhani wananipenda na wana matumaini kuwa Mario anaweza kubadilika na tufikirie zaidi juu ya kazi yake na mpira"
Boateng huenda akaondoka Italia.
 Kiungo wa AC Milan Kevin-Prince Boateng anatarajiwa kutoa maamuzi yake magumu katika siku zijazo kama ataendelea kucheza soka katika ligi kuu ya nchini Italia Serie A au kuondoka, kufuatia kitendo cha kibaguzi alicho fanyiwa wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Pro Patria mwishoni mwa juma.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ghana Boateng pamoja na wachezaji wenzake wa Milan waliamua kuondoka uwanjani kufuatia kitendo hicho kilichofanywa na mashabiki.
Shirikisho la soka la Italia (FIGC) limesema litaendesha uchunguzi, wakati ambapo kitendo cha kususia kuendelea na mchezo huo kuonekana kuwavutia watu wengi mashuhuri akiwemo kocha wa timu ya taifa ya Italia Cesare Prandelli.
Boateng ambaye ana mkataba mpaka 2014, anafikiria kuondoka nchini Italia.
Amenukuliwa na gazeti la Bild la nchini Italia Bouteng mchezaji huyo mzaliwa wa Ujerumani akisema
"hili si jambo la mzaha, nipe siku tatu nilale niamke na nikutane na wakala wangu Roger Wittmann wiki ijayo tuone kama kama kuna haja ya kuendelea kucheza Italia"

No comments:

Post a Comment