Saturday, January 5, 2013

RAIS TOGO KUM'BEMBELEZA ADEBAYOR.


RAIS wa Togo, Faure Gnassingbe amepanga kukutana na nahodha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Emmanuel Adebayor kufuatia mgomo wa mchezaji kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ili kudai posho zao kwa Shirikisho la Soka la nchi hiyo-TFF. Wizara ya Michezo ilitoa taarifa hizo juzi kwamba Adebayor ambaye anacheza katika klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza alitegemewa kutua wakati wowote katika mji mkuu wan chi hiyo Lome kuzungumza na mkuu wa nchi, kitendo ambacho wachambuzi wa soka nchini humo wamesema kinaweza kubadilisha msimamo wa nyota huyo. Togo inapambana na Niger jijini Niemey leo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano hiyo ya Afrika ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 19 mwaka huu nchini Afrika Kusini. Kiungo mkabaji Alaixys Romao anayecheza katika klabu ya Lorient ya Ufaransa amerejea katika kikosi cha nchi hiyo wakati golikipa chaguo la kwanza katika kikosi cha kocha Didier Six bado amekataa kujiunga na wenzake mpaka tatizo la Adebayor litakapotatuliwa. Togo itaanza kampeni zake katika michuano hiyo kwa kupambana na Ivory Coast ambao wote wanatoka magharibi mwa Afrika katika kundi D jijini Rustenburg.

No comments:

Post a Comment