Tuesday, February 5, 2013

AFCON 2013: NUSU FAINALI: NIGERIA v MALI & GHANA v BURKINA FASO!


AFCON_2013-NA_KABUMBU_LIANZE>>BAADA VIPIGO: DROGBA: ‘NIGERIA BINGWA’, ADEBAYOR AMPONDA KOCHA TOGO!
WAKATI NUSU FAINALI za Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, zikitarajiwa kuchezwa Jumatano  huko Nchini Afrika Kusini, Masupastaa wa Afrika, Didier Drogba wa Ivory Coast na Emmanuel Adebayor wa Togo, ambao Timu zao zilinyukwa Robo Fainali na kutupwa nje, wameibuka na kuongea kuhusu michuano hiyo huku Drogba akiisifia Nigeria iliyowafunga lakini Adebayor yeye amemzukia Kocha wao Didier Six na kumtwisha lawama.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
NUSU FAINALI
Jumatano Februari 6
Ghana v Burkina Faso [Mbombela Stadium, Nelspruit Saa 12 Jioni]
Mali v Nigeria [Moses Mabhida Stadium, Durban Saa 3 na Nusu Usiku]
MSHINDI wa TATU
Jumamosi Februari 9
[Nelson Mandela Bay Stadium, Port Elizabeth Saa 3 Usiku]
FAINALI
Jumapili Februari 10
[Soccer City, Johannesburg Saa 3 Usiku]
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Drogba, baada ya kuchapwa 2-1 na Nigeria kwenye Robo Fainali hapo Jumapili, ameisifia Nchi hiyo na kusema imekuwa ikipanda kiwango Mechi hadi Mechi na Timu hiyo inaweza kutwaa Ubingwa wa Afrika.
Drogba ametamka: “Nimevutiwa na Nigeria walipotufunga. Walifanya kazi ngumu na kubwa na wamejitayarisha vizuri. Sidhani kama kuna Timu itaisimamisha Nigeri!”
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
WAMEFIKAJE NUSU FAINALI:
GHANA:
Makundi:
-Ghana 2 Congo DR 2
-Ghana 1 Mali 0
-Niger 0 Ghana 3
Robo Fainali:
-Ghana 2 Cape Verde 0 
BURKINA FASO:
Makundi:
-Nigeria 1 Burkina Faso 1
-Burkina Faso 4 Ethiopia 0
-Burkina Faso 0 Zambia 0
Robo Fainali:
-Burkina Faso 1 Togo 0 [Dakika 120 za Mchezo]
MALI:
Makundi:
-Mali 1 Niger 0
-Ghana 1 Mali 0
-Congo DR 1 Mali 1
Robo Fainali:
-Afrika Kusini 1 Mali 1[Mali yashinda Penati 3-1]
NIGERIA:
Makundi:
-Nigeria 1 Burkina Faso 1
-Zambia 1 Nigeria 1
-Ethiopia 0 Nigeria 2
Robo Fainali:
-Ivory Coast 1 Nigeria 2
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Nae Nahodha wa Togo, Emmanuel Adebayor, amemvaa Kocha wa Timu yao, Didier Six, na kudai Kocha huyo hakuwa na maamuzi mazuri na uendeshaji wa Timu ulikuwa hauridhishi.
Togo walitolewa kwenye Robo Fainali na Burkina Faso baada ya kuchapwa 1-0 katika Dakika 120 za Mchezo na Adebayor amesema: “Kocha hatukusaidia. Mie nilikuwa Uwanjani sasa siwezi kucheza na kuwa Kocha. Nilijitihidi sana lakini yeye hatukusaidia!”
Jumatano, Nusu Fainali zote mbili za AFCON 2013 zitachezwa kwa Ghana kucheza na Burkina Faso Uwanja wa Mbombela huko Nelspruit na kufuatiwa na Mechi kati ya Mali na Nigeria kwenye Moses Mabhida Stadium Mjini Durban.

No comments:

Post a Comment