KLABU ya Arsenal inaweza
kupoteza kiasi cha paundi milioni 30 kwa mwaka wanazopata kutoka kwa
wadhamini wao Emirates kama klabu hiyo ikishindwa kupata nafasi ya
kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Meneja
wa klabu hiyo Arsenal Wenger ameiongoza kushiriki michuano hiyo kila
msimu toka amechukua mikoba ya kuinoa ya kuinoa timu hiyo. Lakini
hivi sasa Arsenal inakabiliwa na msimu mgumu chini ya kocha huyo
Mfaransa na wako katika hatari ya kukosa taji lolote katika kipindi cha
miaka nane mfululizo huku wakiwa bado wanapigania nafasi nne za juu ili
washiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Emirates
wadhamini wa klabu hiyo ambao wako katika mazungumzo ya kuongeza
mkataba mpaka msimu wa mwaka 2014-2015 wameamua kuionya klabu hiyo kwa
kuchukua tahadhari kama ikishindwa kushiriki michuano ya klabu bingwa. Kwasasa
Arsenal wako katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu nchini
Uingereza lakini kuna uwezekano mkubwa wa kutoka katika nafasi hiyo kama
Chelsea ambao walikuwa katika michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia
iliyofanyika Japan wakishinda mechi zao mbili za viporo walizonazo.
No comments:
Post a Comment