Tuesday, February 5, 2013

SKANDALI UPANGAJI MATOKEO: LIVERPOOL YAKANUSHA KUFUATWA NA EUROPOL!!

PAKA_WA_ANFIELD
>>MECHI LIVERPOOL v DEBRECEN SEP 16, 2009 MIONGONI MWA MECHI 680 ZINAZOSHUKIWA KUPANGWA!!
KLABU ya Liverpool imesema wao hawajawahi kuongea na EUROPOL, Polisi wa Kimataifa Ulaya, kuhusiana na uchunguzi wao wa Mechi 680 zenye mashaka ya Matokeo yake kupangwa ingawa jana Mechi yao na Debrecen ilitajwa kuwa ni miongoni mwa Mechi tata katika Skandali kubwa ambalo limeitikisa Ulaya huku FA, UEFA na FIFA zote zikidai hawakuwa na habari yeyote kuhusu Uchunguzi wa EUROPOL.
++++++++++++++++++++++++
EUROPOL=UCHUNGUZI WAO:
-Ulianza Miezi 18 iliyopita:
Ulianzia Germany, Finland na Hungary na kusambaa Nchini Slovenia na Austria.
-Walichunguza Mechi 680 katika Nchi 30:
Barua Pepe 13,000 zilichunguzwa.
-Watuhumiwa 425 walitambuliwa:
Watu 50 wamekamatwa.
-Hati za Upekuzi 80 zilitolewa:
Katika kusaka ushahidi, Hati za Upekuzi 80 zilitolewa.
++++++++++++++++++++++++
Katika Mechi hiyo ya Liverpool na Debrecen ya UEFA CHAMPIONZ LIGI iliyochezwa Tarehe 16 Septemba 2009 na Liverpool kushinda kwa Bao 1-0 Mfungaji akiwa Dirk Kuyt, inadaiwa kuna Kundi la Wahalifu wa Mashariki ya Mbali huko Asia walimuhonga Kipa wa Debrecen, Vukasin Poleksic, aachie Bao 3 ili wazoe Mihela kwenye Kamari.
Lakini Kipa huyo wa Klabu hiyo ya Hungary alikuja kunaswa baadae kwa kuhusishwa na kupanga Matokeo katika Mechi kati ya Debrecen na Fiorentina ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambao wote walikuwa Kundi moja na Liverpool Mwaka huo 2009 na Kipa huyo akafungiwa Miaka Miwili kwa Kosa hilo.
EUROPOL wamekuwa wakiendesha uchunguzi wao kwa Miezi 18 na Mechi pekee kwa Klabu ya England kuchunguzwa ni hiyo ya Liverpool na pia zipo Mechi za Kombe la Dunia, Mechi za Mchujo Ulaya na baadhi ya Ligi za Ulaya.
Inadaiwa Wapangaji wa Matokeo Mechi ni Wahalifu kutoka Asia ambao wanawarubuni Wachezaji na Marefa kupoteza Mechi ili wao wanufaike kwa Uchezaji Kamari.

No comments:

Post a Comment