Friday, January 18, 2013

WENGER AKIRI KUMHUSUDU CAVANI AJE KATIKA DIMBA LA EMIRATES .


MENEJA wa klabu ya Arsenal Arsenal Wenger amekiri kuwa anamhusudu mshambuliaji wa klabu ya Napoli Edinson Cavani lakini kocha atalazimika kubadili mfumo wa matumizi ya fedha wa klabu hiyo kama atataka kumsajili mchezaji huyo. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Wenger alikiri kumhitaji mchezaji huyo ambaye ni raia wa Uruguay na kusema kwamba atawagharimu pesa nyingi kama wakiamua kumfukuzia ili wamsajili. Kama Arsenal itamhitaji mchezaji huyo italazimika kulipa kiasi cha paundi milioni 52 kama ada ya uhamisho huku wakilazimika kumlipa mshahara wa paundi 150,000 kwa wiki katika mkataba wa miaka anaoutaka. Malipo hayo yatakuwa yamevunja rekodi ya klabu hiyo ambayo kwasasa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi ni Lukas Podolski anayepokea kiasi cha paundi 90,000 wakati usajili uliovunja rekodi ulikuwa ni ule wa Andrey Arshavin aliyenunuliwa kwa paundi milioni 15 kutoka klabu ya Zenit St Petersburg ya Urusi.

No comments:

Post a Comment