Tuesday, February 5, 2013

WACHEZAJI TENISI WANAHITAJI KUPIMWA DAMU ZAIDI.


MCHEZAJI nyota wa mchezo wa tenisi, Andy Murray anataka wadau wa mchezo huo kujifunza kutokana na kashfa ya utumiaji dawa za kuongeza iliyomkumba Lance Armstrong kwa kuongeza umakini kwenye suala hilo. Murray anaamini kuwa zawadi zinazotolewa katika mchezo huo zinaweza kupunguzwa kama ndio njia pekee ya kuwezesha wachezaji wa mchezo huo kupata vipimo vya damu mara kwa mara ili kulinda hadhi ya mchezo huo. Nyota huyo anayeshika namba tatu katika orodha za ubora duniani amesema hiyo ni juu ya Shirikisho la Tenisi la Kimataifa kuwekeza fedha zaidi ili kuhakikisha vipimo zaidi vinafanyika na kuepukana na kashfa zozote za utumiaji dawa za kuongeza nguvu. Daktari mmoja wa Hispania aitwaye Eufemiano Fuentes kwasasa ana kesi jijini Madrid baada ya kukiri kuwasaidia wanamichezo kuwapa dawa zilizokatazwa michezoni. Shirika la Kimataifa linapambana na matumizi ya dawa hizo michezoni lilidai kuwa wachezaji wa tenisi ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa wateja wa Fuentes wakati mpango wake huo ulipostukiwa na polisi nchini Hispania mwaka 2006.

No comments:

Post a Comment