Saturday, December 29, 2012

BARCA: KOCHA VILANOVA KURUDI JANUARI

>>BAADA KUFANYIWA OPERESHENI KUTIBU KANSA!
BARCA_v_REALRAIS wa FC Barcelona, Sandro Rosell, amesema kuwa Kocha wao Mkuu, Tito Vilanova, atarejea kazini baada ya Siku 15 hadi 20 kufuatia upasuaji ili kutibu Kansa iliyomrudia tena.
Vilanova, Miaka 44, alifanyiwa operesheni hiyo Desemba 20 kujaribu kuganga Kansa ya Tezi ambayo mara ya kwanza aliipata Mwaka 2011 na kutibiwa na hivi karibuni ikarudi tena.
Rosell amesema: “Atarudi baada ya Siku 15 au 20 lakini Siku nyingine itabidi awe Hospitalini kwa matibabu. Atachanganya kazi na matibabu.”
Chini ya Vilanova, ambae alitwaa himaya mwishoni mwa Msimu uliopita baada ya Kocha Pep Guardiola kung’atuka, Barcelona imeweka Rekodi ya kuanza vyema La Liga kwa kupoteza Pointi mbili tu katika Mechi 17 za Ligi hiyo ambayo wanaoongoza kwa Pointi 9.
Kwa sasa Barcelona wanasimamiwa na Msaidizi wa Vilanova, Jordi Roura, lakini Msimu wa Soka huko Spain upo kwenye Vakesheni ya Krismasi na Mwaka mpya na Mechi inayofuata kwa Barcelona ni Dabi ya Jiji la Barcelona dhidi ya Espanyol hapo Januari 6.
LA LIGA:
**LIGI MAPUMZIKONI HADI JANUARI 6
MSIMAMO-Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 17]
1 Barcelona Pointi 49
2 Atletico Madrid 40
3 Real Madrid 33
4 Malaga 31
5 Real Betis 28
6 Levante 27
7 Real Sociedad 25
RATIBA:
Jumapili Januari 6
3:00 FC Barcelona v RCD Espanyol
3:00 Celta de Vigo v Real Valladolid
3:00 Deportivo La Coruna v Malaga CF
3:00 Real Mallorca v Atletico de Madrid
3:00 Real Madrid CF v Real Sociedad
3:00 Rayo Vallecano v Getafe CF
3:00 Sevilla FC v Osasuna
3:00 Real Zaragoza v Real Betis
3:00 Levante v Athletic de Bilbao
3:00 Granada CF v Valencia

No comments:

Post a Comment