Saturday, February 2, 2013

JULIO ASEMA YANGA NA AZAM WANA POINTI ZA SIMBA, PIGA UA KOMBE LINABAKI MSIMBAZI


Kocha wa Simba, Jamhuri Kihwelo akizungumza na Waandishi wa Habari mchana huu Msimbazi. Kulia ni Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ezekiel Kamwaga.


KOCHA Msaidizi wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC, Jamhuri Mussa Kihwelo amesema kwamba Yanga wana pointi zao tatu sawa na Azam, hivyo hawana shaka ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwishoni mwa msimu.  
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa mikutano wa klabu ya Simba SC, Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam mchana wa leo, Jamhuri maarufu kama Julio alisema kwamba kwa sasa wanazidiwa pointi sita na Yanga, lakini anaamini mwisho wa msimu watatetea ubingwa wao tu.
“Tutawafunga Yanga na kuchukua pointi tatu, tutawafunga Azam FC na kuchukua pointi tatu na sisi tunajua Yanga na Azam watafungwa pia mechi nyingine na sisi tutashinda zote na kupanda kileleni,”alisema Julio.
Kwa sasa katika msimamo wa Ligi Kuu, Yanga wapo kileleni kwa pointi zao 32, wakifuatiwa na Azam yenye pointi 30, wakati Simba SC ina pointi 26.
Jamhuri alisema kwamba Simba inaendelea vizuri na maandalizi yake ya mchezo wa keshokutwa dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na wana matumaini makubwa ya kushinda.
Beki huyo wa zamani wa Simba SC, alisema anafahamu JKT Ruvu ni timu nzuri na ngumu, lakini hawataweza kuizuia timu yao kubeba pointi tatu hiyo kesho

No comments:

Post a Comment