Saturday, January 12, 2013

WENGER BADO ALIA NA RVP, COLOCCINI AIPIGA CHINI NEWCASTLE!!

>>TEVEZ-CITY YATAFAKARI MKATABA MPYA!!
Wenger aumia na RVP
WENGER_AHIMIZA12Arsene Wenger amekiri kuwa inamsononesha sana kumwona Nyota wake wa zamani wa Arsenal Robin van Persie akiipaisha Manchester United kuelekea kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England.
Man United walimsaini Robin van Persie Mwezi Agosti 2012 kutoka Arsenal kwa Dau la Pauni Milioni 24 na Magoli yake 20  yameisaidia Man United kuwa kileleni mwa BPL, Barclays Premier League, wakiwa Pointi 7 mbele ya Timu ya Pili Man City na Pointi 18 mbele ya Arsenal na hilo limemfanya Wenger akubali Mchezaji huyo ndie atakaepeleka Ubingwa Old Trafford.
Amesema: “Inaumiza sana kuiona Manchester United wako mbali mbele yetu. Unajua ukiwauzia Robin van Persie Manchester United basi wataongoza Ligi.”
Wenger aliongeza: “Robin ni mmoja wa Mastraika Bora Duniani na inajulikana atawafungia Magoli. Yupo kwenye kilele cha Gemu yake! ”
Coloccini
Nahodha wa Newcastle United Fabricio Coloccini ameiambia Klabu hiyo kuwa anataka kuhama Mwezi huu Januari kwa sababu binafsi.
Coloccini, Miaka 30, ambae anatoka Cordoba, Argentina, alisainiwa na Newcastle Mwaka 2008 na kwa Dau la Pauni Milioni 10.3.
Kwenye Dirisha la Uhamisho la Januari, Newcastle tayari ishamuuza Straika wao Demba Ba kwa Chelsea.
Tevez
Manchester City inatafakari uwezekano wa kumuongezea Mkataba Mchezaji wao Carlos Tevez ili kumzuia asiondoke bure bila malipo Mkataba wake wa sasa utakapomalizika Miezi 18 ijayo.
Tevez, ambae alisaini Mkataba wa Miaka mitano na Man City Mwaka 2009, hajaamua chochote kuhusu hatima yake lakini inaaminika anataka kurudi kwao Argentina kuichezea Boca Juniors, Klabu ambayo alianza kucheza Soka.
Akiongelea kuhusu Tevez, Mancini alisema: “Sijui Carlos anafikiria nini. Bado tuna Miezi 18 na muda upo wa kuongea nae.”
+++++++++++++++++++++++
BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA:
Jumamosi 12 Januari 2013
[SAA 12 Jioni]
Aston Villa v Southampton
Everton v Swansea
Fulham v Wigan
Norwich v Newcastle
Reading v West Brom
Stoke v Chelsea
Sunderland v West Ham
Jumapili 13 Januari 2013
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Man United v Liverpool
[SAA 1 Usiku]
Arsenal v Man City
Jumatatu 14 Januari 2013
[SAA 5 Usiku]
QPR v Tottenham

No comments:

Post a Comment