Saturday, February 2, 2013

FERGIE AKANA SHITAKA LA FA!!


>>AOMBA AWASILISHE UTETEZI KIMAANDISHI, FA KUAMU NINI KINAFUATA!!
FERGIE_KAZINISIR ALEX FERGUSON mekana Shitaka alilofunguliwa na FA, Chama cha Soka England, kufuatia kauli yake kuhusu Refa Msaidizi baada ya Timu yake Manchester United kutoka sare 1-1 na Tottenham kwenye Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Januari 20 Uwanjani White Hart Lane.
Ferguson alimyooshea kidole Refa Msaidizi Simon Beck kwa kushindwa kuashiria Penati baada ya Straika wake Wayne Rooney kuangushwa ndani ya Boksi.
Mara baada ya kauli ya Ferguson, FA ilimtaka Meneja huyo kujieleza na ikaamua kufungua Mashitaka rasmi na alipewa hadi Ijumaa Saa 1 Usiku, Bongo Taimu, kuyajibu.
Kauli ambazo zimemtia matatani Ferguson ni pale alipotamka: “Kulikuwa hamna njia Mshika Kibendera angeweza kutoa ile [Penati!]-aliwapa kila kitu! Kilikuwa kitu cha wazi na alikuwa Yadi 10 au 12 na hakutoa! Wao walipewa kila kitu!”
Pia alikumbushia tukio ambalo Refa Msaidizi Simon Beck alipowakatili Man United Aprili 2010 walipofungwa 2-1 na Chelsea kwa Mshika Kibendera huyo kutokutoa Ofsaidi ya wazi dhidi ya Didier Drogba aliefunga Bao la ushindi.
Akikana Mashitaka hayo, Ferguson aliomba awasilishe Ushahidi wake Kimaandishi na sasa FA itatathmini majibu yake na kuamua kama impe Adhabu ya Kufungiwa Mechi na Faini au mojawapo.
Kihistoria, Ferguson na FA wana misuguano ya muda mrefu na Machi 2011 alifungiwa Mechi 5 na kupigwa Faini Pauni 30,000 kwa kumtuhumu Refa Martin Atkinson kwa kuipendelea Chelsea.

No comments:

Post a Comment