Pigo: Iker Casillas akiugulia maumivu ya mkono ambayo huenda yakamuweka nje dhidi ya Manchester United mwezi ujao. |
Iker
Casillas yuko katika mashaka makubwa ya kuwepo katika kikosi cha Real
Madrid kitakachoshuka dimbani dhidi ya Manchester United mchezo wa ligi
ya vilabu bingwa Ulaya kufuatia taarifa awali kusema kuwa mlinda mlango
huyo wa kimataifa wa Hispania kuvunjika mkono.
Casillas
amepatwa nadhahma hiyo katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Valencia
mchezo wa kombe la mfalme 'Copa del Rey' uliopigwa jumatana ya kusukumwa
na mchezaji mwenzake Alvaro
Arbeloa katika harakati za kuokoa mpira katika eneo la hatari.
Madrid
inatarajia
kutoa maelezo ya ukubwa wa maumivu ya mlinda mlango huyo na aina ya
tiba wakati ambapo Adan Garrido akiwa katika hali ya maandalizi kuziba
pengo la mlinda malango huyo mzoefu namba moja wa Hispania.
Casillas
pia atakosekana katika mchezo wa ligi ya La liga kesho kutwa jumapili
dhidi ya Getafe na mchezo wa marudiano wa Copa Del Rey dhidi ya Valencia
wiki ijayo.
Pia
atakuwa katika vita ya kupigania kurejesha hali yake ya mkono katika
kawaida ili kuwemo katika kikosi kitakachokuwa dimbani Februari 13 dhidi
ya United katika dimba la Santiago Bernabeu.
Taarifa
ya klabu yake imesema baada ya kufanyiwa uangalizi wa awali kupitia
kipimo cha 'x-rays' imethibitika kuwa Iker Casillas amepata mpasuko
mdogo katika mfupa unaotambuliaka kama metacarpal katika mkono wake wa kushoto.
'hiyo italazimu apate uangalizi mwingine kutoka mtaalamu zaidi leo (yaani jana jioni) na kuamua aina gani ya tiba afanyiwe'
Vita? Casillas na meneja wake Jose Mourinho walikuwa katika vita katika siku za hivi karibuni.
Hata
hivyo maumivu makubwa kwa mlinda mlango huyo yanakuja katika kipindi
nyeti cha kusubiri wiki mbili cha kampeni kubwa ya michuano mikubwa ya
vilabu barani ulaya.
Casillas
amerejeshwa katika kikosi cha kwanza baada ya mzozo mkubwa mkubwa baina
yake yeye na Mourinho ulioibuka kipindi cha majira ya baridi ambapo
Mourinho aliamua kumuweka benchi bila sababu ya kueleweka.
Maamuzi ya Mourinho yaliibua hasira kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo na kutiwa utambi na vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment