MENEJA wa klabu ya Real
Madrid Jose Mourinho amesisitiza kuwa hatajiuzulu wadhfa huo pamoja na
timu yake kufungwa mabao 3-2 na Malaga ambao umewafanya kuachwa alama 16
na vinara wa La Liga Barcelona. Kufungwa
kwa Madrid kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na Mourinho kufuatia uamuzi
wake wa kumuacha golikipa ambaye ndiye nahodha wa timu hiyo Iker
Casillas katika kikosi cha kwanza. Akihojiwa
kama anahofu kibarua chake kitakuwa kimefikia ukingoni mara baada ya
mchezo Mourinho amesema hahofii chochote na hawezi kuachia ngazi kwani
kupoteza mechi ni sehemu ya mchezo la msingi ni kujipanga na kuangalia
wapi walikosea. Hiyo
ni mara ya kwanza kwa Casillas katika kipindi cha miaka 10 kupumzishwa
benchi na kumpisha golikipa namba mbili Antonio Adan mwenye umri wa
miaka 25.
No comments:
Post a Comment