Wednesday, January 2, 2013

SAJUKI KUZIKWA IJUMAA KISUTU



Waombolezaji wakiwa kwenye msiba wa Sajuki Tabata jijini Dar es Salaam leo, Januari 2, 2013. 

Msanii wa vivhekesho, Mtanga (kushoto) akiwa na waombolezaji wengine katika msiba wa Sajuki leo Januari 2, 2013.

Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Sajuki leo Januari 2, 2013.

Piga pale...! Sajuki (kulia) akiwa katika maandalizi ya filamu yake mojawapo kali wakati wa enzi za uhai wake.
Hatimaye ule utata kuhusiana na mahala pa kumzika msanii Juma Kilowoko 'Sajuki' umepatiwa jibu baada ya baba yake kukubali kuwa azikwe jijini Dar es Salaam.

Kutokana na uamuzi huo, sasa msanii huyo aliyekuwa nyota na kipenzi cha wengi enzi za uhai wake atazikwa keshokutwa Ijumaa (Januari 4) kwenye makaburi ya Kisutu.

Awali, baba wa msanii huyo alitaka mwanawe akazikwe kwao mkoani Songea. Hata hivyo, baada ya kuketi na kujadili kwa kina na familia yake, akaamua kutangaza kuwa mwanawe huyo kipenzi atazikwa jijini Dar es Salaam ili kutoa nafasi kwa rafiki zake wengi aliokuwa akishirikiana nao katika kazi zake za kila siku za kisanii kupata nafasi ya kushiriki mazishi yake.

Mzee Kilowoko ametoa msimamo huo mpya leo hoo hii, ikiwa ni muda mfupi tu baada ya kutangaza awali kuwa mwanawe atakwenda kuzikwa Songea.

Sajuki amefariki leo asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi na kupumua kwa msaada wa mashine kabla ya kuaga dunia mishale ya saa 1:00 asubuhi.

No comments:

Post a Comment