VILANOVA ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI.
MENEJA wa Barcelona,
Tito Vilanova ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kufanyiwa upauji
kuondoa uvimbe wa kansa uliokuwa umeota kwenye koo. Vilanova
mwenye umri wa miaka 44 alifanyiwa upasuaji huo Alhamisi iliyopita na
kwasasa anakabiliwa na matibabu ya mionzi kwa kipindi cha wiki sita ili
kudhibiti kabisa tatizo hilo linalomkabili. Huo
ni upasuaji wa pili kufanyiwa baada ya ule aliofanyiwa mwaka 2011
kipindi hicho akiwa msaidizi wa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Pep
Guardiola. Barcelona
ilifanikiwa kuifunga Valladolid mabao 3-1 jana usiku na baada ya hapo
Xavi Hernandez ambaye alifunga bao la kwanza amesema wanamzawadia
ushindi huo kocha wao huo ambaye anapitia kipindi kigumu hivi sasa
katika maisha yake. Kwasasa
kocha msaidizi Jordi Roura ambaye amekuwa benchi la ufundi la klabu
hiyo toka mwaka 2009 ndiye aliyekabidhiwa timu wakati wa kipindi hiki
ambacho Vilanova hayupo.
No comments:
Post a Comment