Wednesday, January 16, 2013

KUELEKEA MASHINDANO YA MATAIFA NI MAKOCHA WATATU PEKEE NDIO WALIORUDI KATIKA AFCON.


MAKOCHA watatu pekee ambao walikuwepo katika michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon mwaka mmoja uliopita ndio wamerejea katika michuano ya mwaka huu inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi. Mmojawapo ni Mfaransa Herve Renard ambaye aliiongoza Zambia kupata mafanikio ya kushangaza jijini Libreville Februari mwaka jana na kuendelea kukinoa kikosi cha nchi hiyo pamoja na kazi China na Mashariki ya Kati. Sami Trabelsi anayefundisha Tunisia ni kocha mwingine ambaye anarejea na timu hiyo huku akiomba kupata matokeo mazuri zaidi baada ya kuifikisha nchi hiyo Robo fainali katika fainali zilizofanyika Gabon na Equatorial Guinea mwaka jana. Mwingine ni Mjerumani Gernot Rohr, ingawa hakuongezewa mkataba na wenyeji wenza wa michuano ya mwaka jana Gabon baada ya kufungwa katika mchezo war obo fainali lakini alipewa mikoba ya kuinoa Niger na kufanikiwa kuipeleka nchini Afrika Kusini kwenye michuano hiyo. Katika orodha ya makocha waliopo Afrika Kusini inajumuisha makocha nane kutoka Ulaya, saba wa Afrika na mmoja kutoka Amerika Kusini.

No comments:

Post a Comment