Wednesday, January 16, 2013

IOC YATARAJIA KUMNYANG'ANYA MEDALI ARMSTRONG.


MWENDESHA baiskeli Lance Armstrong anatarajiwa kuirejesha medali ya Olimpiki mara mahojiano yake ya kukiri kutumia dawa za kuongeza nguvu michezoni yatakaporushwa hewani kesho. Armstrong ambaye amekuwa akikana kutumia dawa hizo kwa miaka mingi ameandikiwa barua na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa-IOC baada ya kukiri katika kipindi kinachoendeshwa na mtangazaji maarufu wa Marekani, Oprah Winfrey kutumia dawa hizo. Mjumbe wa IOC, Dick Pound ambaye pia amewahi kuwa kiongozi wa Shirikika la Kupambana na Dawa za Kuongeza Nguvu-WADA amesema ni wajibu wa IOC nao kuchukua hatua juu ya suala la Armstrong ndio maana wamemuandikia barua ya kumtaka kurejesha medali yao. Pamoja na kwamba mazungumzo hayo bado hayajarushwa hewani lakini Winfrey mwenyewe amethibitisha kuwa Armstrong mwenye umri wa miaka 41 amekubali kudanganya kwa kutumia dawa hizo. Armstrong alinyang’anywa mataji saba ya michuano ya baiskeli ya Toure de France baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa hizo na WADA lakini alikuwa hajazungumza lolote toka akumbwe na sakata hilo.

No comments:

Post a Comment