Wednesday, January 16, 2013

ZAHOR PAZI ATIMKIA AFRIKA KUSINI KUJARIBIWA


Zahor Pazi
KIUNGO mshambuliaji wa mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC, Zahor Iddi Pazi ameondoka leo Alfajiri Dar es Salaam kwenda Afrika Kusini kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya Blomomfontein Celtic ya nchini humo.
Baba mzazi wa mchezaji huyo, ambaye Desemba ametolewa kwa mkopo katika klabu ya JKT Ruvu Pwani, amesema  kwamba kijana wake huyo amepatiwa nafasi hiyo na klabu yake ya Azam.
“Alipokuwa Kongo (DRC) na Azam kwenye Kombe la Hisani kuna wakala alivutiwa na kipaji chake akaomba apelekwe kufanya majaribio, basi wakati umefika ameondoka leo,”alisema.
Zahor licha ya kuwa mchezaji mzuri amekuwa hana bahati ndani ya kikosi chs Azam tangu asajiliwe msimu uliopita.
Mwanzoni mwa msimu, Zahor aliomba kwenda kucheza kwa mkopo Coastal Union ya Tanga, lakini uongozi wa klabu hiyo ukamkatalia kabla ya kumtoa kwa mkopo Desemba mwaka jana.

No comments:

Post a Comment