Michael Richard Wambura |
Aliyewahi
kuwa katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF Michael Richard
Wambura na baadaye kukutana na vizingiti lukuki kila alipokuwa
anajitokeza kuwania uongozi wa mpira katika ngazi mbalimbali, hii leo
amejitokeza tena kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya makamu wa Rais wa
shirikisho hilo.
Akionekana
ni mwenye matumaini makubwa mara hii na maamuzi yake hayo, Wambura
amesema kwasasa amekamilisha jukumu la kwanza la kuchukua fomu kama raia
mwenye haki ya kufanya hivyo na kwamba mikakati ya kuelekea katika
mchakato mzima wa uchaguzi kwa upande wake ndio unaanzia hapo.
Amesema
angependelea zaidi watanzania zaidi wangejitokeza kuchukua fomu ili
kuleta changamoto kubwa zaidi katika mchakato mzima wa uchaguzi huo.
Amempongeza
Rais wa sasa Leodigar Tenga kwa kuamua kuachia nafasi hiyo na kwamba
hiyo inaonyesha ni namna gani Rais Tenga alivyo muumini mzuri wa vipindi
na kuruhusu mawazo mapya na mfumo mpya na watu wapya ili kumpokea
nafasi yake.
Michael Wambura akiongea na waandishi wa habari. |
Amesema
unapokuwa madarakani yapo ambayo utayafanikisha na mengine mazuri watu
wayaenzi na yale aliyoshindwa wengine watayapokea kuanzia hapo na
kuyaendeleza.
Amesema
sababu ambazo zimemfanya kuchukua fomu hii leo siyo za wakati ule na
kwamba kila jambo linawakati wake na pengine sababu ambazo zilikuwa
zikionekana ni tatizo kwa wakati ule huenda zisiwe hivyo kwasasa.
Wambura
amedokeza sababu zilizo msukuma kuwania nafasi hiyo ya makamu wa Rais
kwakuwa ni nafasi ambayo inachangamoto nyingi na kwamba kuna mengi
ambayo hayajafanyiwa kazi kwa kuwa nafasi hiyo haijapata mtu muafaka na
kwamba wale wanaomaliza muda wao wanahitaji kusaidiwa.
Ameizungumzia pia sifa ya Rais ajaye kuwa anatakiwa kuwa amechaguliwa kwa mujibu wa katiba na kuupenda mpira wa miguu.
Awe
ni mwenye kuelewa kuwa mpira wa miguu unatakiwa kuchezwa nchi nzima kwa
kuwa ni mchezo unaopendwa na wengi kote nchini, vilevile awe na muda wa
kuushughulikia mchezo wa soka na mwenye kiu ya maendeleo ya soka.
Amesema
kuna haja ya kubadilisha mfumo wa soka uliopo ili kuwa na mpira ulio
bora, timu ya taifa bora na kutoa nafasi kwa walio wengi kuucheza mpira
wa miguu.
Wambura
aliwahi kugombea nafasi ya mwenyekiti mkoa wa mara lakini alienguliwa
kutokana na kamati ya uchaguzi kusema kuwa hakuwa muadilifu kabla ya
kutaka kujaribu tena bahati yake katika chama cha soka mkoa wa Dar es
Salaam DRFA ambapo baadaye aliamua kujitoa na kuelekea katika kamati ya
rufaa inayoongozwa na Profesa Mgongo Fimbo ambayo ilimsafisha.
Hata
hivyo TFF ilipinga maamuzi hayo na kuelekea shirikisho la soka duniani
fifa kuomba mwongozo ambapo FIFA ambalo liliagiza TFF kuunda kamati ya
rufaa inayojitegemea ambapo kwasasa mabadiliko hayo yamefanyika.
Kwasasa Wambura yuko safi baada ya maamuzi ya kamati ya rufaa ya Prof Mgongo Fimbo.
No comments:
Post a Comment