Wednesday, January 16, 2013

ROBO FAINALI-COPA del REY: Real 2 Valencia 0, COPPA ITALIA: Inter 3 Bologna 2

>>COPA del REY: LEO BARCA v MALAGA!
BARCA_v_REALReal Madrid wamejiweka kwenye mazingira mazuri ya kutinga Nusu Fainali ya COPA del REY baada ya jana kuichapa Valencia Bao 2-0 katika Mechi ya kwanza ya Robo Fainali iliyochezwa Uwanjani Santiago Bernabeu.
Karim Benzema ndie alieipatia Real Bao la kwanza katika Kipindi cha Kwanza na Andrés Guardado kujifunga mwenyewe katika Dakika ya 74 na kuipa Real ushindi wao Bao 2-0 ambao watakwenda nao ugenini kurudiana na Valencia Wiki ijayo.
Katika Mechi hiyo, Kipa wa Valencia, Vicente Guaita, alimkatili Nyota Cristiano Ronaldo mara mbili kwa kuokoa magoli ya wazi.
Mshindi kati ya Valencia na Real atacheza na Mshindi kati ya Barcelona na Malaga ambao leo wanacheza Mechi yao ya kwanza ya Robo Fainali.
Mechi nyingine ya Robo Fainali itakayochezwa leo ni kati ya Real Zaragoza na Sevilla na Alhamisi ni Atlético Madrid na Real Betis.

COPA del REY
ROBO FAINALI
MATOKEO/RATIBA
Jumanne Januari 15
Real Madrid CF 2 Valencia 0
Jumatano Januari 16
[SAA 3 na Nusu Usiku]
Real Zaragoza v Sevilla FC
[SAA 5 na Nusu Usiku]
Barcelona v Malaga
Ijumaa Januari 18
[SAA 6 Usiku]
Atletico Madrid v Real Betis
Jumatano Januari 23
MARUDIANO
Sevilla FC v Real Zaragoza
Valencia v Real Madrid CF
Malaga v Barcelona
Real Betis v Atletico Madrid

COPPA ITALIA: Inter 3 Bologna 2
Inter Milan, wakicheza kwao Stadio Giuseppe Meazza Mjini Milano, jana walitinga Nusu Fainali ya COPPA ITALIA lakini nusura wapokwe tonge mdomoni baada ya kuongoza 2-0 na Bologna kusawazisha katika Dakika 9 za mwisho lakini wakaibuka kidedea baada ya Bao la Sekunde ya mwisho ya Dakika 30 za nyongeza kuwapa ushindi wa 3-2.

MAGOLI:
Inter Milan 3
-Fredy Guarín Dakika ya 34
-Rodrigo Palacio 77
-Andrea Ranocchia 120
Bologna 2
-Alessandro Diamanti Dakika ya 81
-Manolo Gabbiadini 84

Beki Andrea Ranocchia ndie aliefunga Bao la 3 na la ushindi katika Dakika ya 120 na sasa watacheza Nusu Fainali na Mshindi kati ya  AS Roma au Fiorentina wanaokutana Jumatano Usiku.
Nusu Fainali nyingine ni kati ya Mabingwa wa Italy Juventus na Lazio.

COPPA ITALIA
ROBO FAINALI
RATIBA:
Jumatano Januari 16
[SAA 5 Usiku]
Fiorentina v AS Roma
NUSU FAINALI:
Jumanne Januari 22
SS Lazio v Juventus
Jumanne Januari 29
Juventus v SS Lazio

No comments:

Post a Comment