Wednesday, January 16, 2013

KIKAPU YAPATA KOCHA MSAIDIZI WA TIMU YA TAIFA JOCQUIS SCONIERS

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiZxCdDa0_cJ6PVmfn3CjEkzNRnnK1t5jRPLkVh5LIBe2zxRKwMnojdWmgHorhuzIinkPY4BNV_66uRkAHsFutx30wUBsmTq0Tjekz6tNDApb3U5bpM127mCtmWs29E4v6p4e24p5tC_H8/s1600/IMG00988-20121102-1956.jpg

Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya mpira wa kikapu, Jocquis Sconiers   anatarajiwa kuanza kazi ya kuinoa timu ya taifa ya wanawake na wanaume ya mchezo huo kwenye uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Sconiers ametua nchini huku akiwa na mikakati kadhaa aliyodai kuwa ikitekelezwa vyema, mchezo wa mpira wa kikapu nchini utsonga mbele kwa kiasi kikubwa na pengine  kuzipiku timu za mataifa ya jirani kama Kenya na Uganda.


Hata hivyo, kocha huyo amebakiwa na wiki moja tu kuinoa timu hiyo kabla ya kuanza kwa michuano ya mchezo huo ya Kanda ya Tano ya Afrika itakayofanyika jijini Dar es Salaam.

  Katibu msaidizi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Michael Maluwe, amesema wamefurahishwa na ujio wa kocha huyo na kuwataka wadau kumpa ushirikiano.

"Tunaomba wachezaji na wadau wa kikapu nchini wampe ushirikiano ili afanye kazi yake vizuri na kusaidia timu zetu," aliongeza  Maluwe.


Aliwataja baadhi ya wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho kuwa ni Ladislaus Ikungura,Gerald Baru, Abdallah Ramadhani ‘Dulla’, Henry Mwinuka ‘kidume’ na

Sudi Abdulrazak.

Wengine ni Sylivian Yunzu (Maige), Mussa Chacha, Frankline Simkoko,Small Forward, Mohamed Ally ‘Dibo’, Amir Muhidin Saleh na nahodha, Lusajo Samwel.


Kocha Bahati Mgunda alisema katika timu ya wanaume alikuwa na wachezaji 32 lakini sasa wamechujwa na kubaki 18 ambao watatu kati yao watapunguzwa zaidi na kubaki 15.

No comments:

Post a Comment