Wednesday, January 16, 2013

FA CUP-MARUDIANO RAUNDI YA 3: LEO ARSENAL, MAN UNITED ZASAKA KUSONGA!!

FERGIE_n_WENGER-KICHEKO>>DONDOO ZA MECHI: MAN UNITED v WEST HAM, ARSENAL v SWANSEA
BAADA ya kwenda sare ugenini za 2-2, Vigogo Manchester United na Arsenal, Klabu ambazo ndizo zinashika Rekodi ya kutwaa FA CUP mara nyingi, leo Usiku kila mmoja atakuwa Uwanja wa nyumbani kucheza Mechi za marudio, ManUnited Uwanjani Old Trafford dhidi ya West Ham, na Arsenal, ndani ya Emirates, kuivaa Swansea City.
ZIFUATAZO ni TAARIFA fupi za Mechi hizo:
MAN UNITED v WEST HAM
Uwanja: Old Trafford
Tarehe: Jumatano, Januari 16
SAA: 5 Dak 5 Usiku
Hali za Wachezaji
Wayne Rooney anatarajiwa kuichezea Manchester United Mechi yake ya kwanza tangu Siku ya Krismasi alipojiumiza Goti mazoezini.
Pia Winga Nani anategemewa kuwemo kwenye Kikosi baada ya kupona Musuli za Paja zilizomfanya azikose Mechi 15 zilizopita.
Mchezaji pekee ambae ni Majeruhi kwa Man United ni Ashley Young alieumia Goti Jumapili iliyopita walipocheza na Liverpool.
Majeruhi wa West Ham ni James Collins, Mark Noble, George McCartney, Joey O'Brien na Andy Carroll huku  Modibo Maiga ametimka kwenda kuichezea Mali kwenye AFCON 2013 na pia Wachezaji wao wapya waliosainiwa Mwezi huu Jnuari, Wellington Paulista na Marouane Chamakh , hawaruhusiwi kucheza Raundi hii.
Uso kwa Uso
-Manchester United imeshinda Mechi 8 kati ya 10 walizocheza mwisho na West Ham na Mwezi Novemba, kwenye Mechi ya Ligi Kuu England, waliifunga West Ham 1-0 kwa Bao la Sekunde ya 33 la Robin van Persie.
Rekodi
Manchester United
-Wametinga Fainali za  FA CUP 18 na kushinda 11, huku 5 zikiwa chini ya Sir Alex Ferguson.
West Ham United
-Walitwaa FA CUP Miaka ya 1964, 1975 na 1980 winners na mara ya mwisho kutinga Fainali ni Mwaka 2006 lakini katika Misimu mitano iliyopita walishindwa kusonga zaidi ya Raundi ya 3 mara 3.
ARSENAL v SWANSEA
Uwanja: Emirates Stadium
Tarehe: Jumatano, Januari 16
SAA:  4 Dak 30 Usiku
Hali za Wachezaji
Arsenal watawakosa Laurent Koscielny na Mikel Arteta wakati  Koscielny akiwa Kifungoni na Kiungo Arteta akiwa majeruhi.
Meneja wa Swansea, Michael Laudrup, ana Kikosi chake kamili bila dosari yeyote ispokuwa Mchezaji mpya wa Mkopo, Roland Lamah, ambae usajili wake ulichelewa kwa ajili ya Mechi hii.
Uso kwa Uso
-Arsenal wameshinda Mechi 6, Sare 2 na kufungwa 5 katika Mechi 13 za mwisho walizocheza na Swansea.
Rekodi
Arsenal
-Arsenal wapo kwenye Rekodi ya kuwa Timu ya Pili kwa kutwaa FA CUP mara nyingi, wametwaa mara 10 wakiwa nyuma ya Manchester United waliolibeba mara 11 katika Fainali 17 walizoshiriki ukilinganisha na 18 za Man United.
-Chini ya Arsene Wenger, Arsenal wametwaa FA CUP mara 4 na mara ya mwisho ni Mwaka 2005.

No comments:

Post a Comment