Wednesday, January 16, 2013

NADAL KUREJEA MICHUANO YA ATP BRAZIL OPEN.


MCHEZAJI tenisi nyota wa Hispania, Rafael Nadal ambaye yuko nje ya uwanja kuanzia katikati ya msimu uliopita kwa sababu ya majeruhi anatarajia kurejea tena mwezi ujao katika michuano ya ATP Brazil Open itakayofanyika jijini Sao Paulo baada ya kupona kabisa. Ofisa habari wa Nadal, Benito Perez-Barbadillo alithibitisha taarifa za nyota huyo anayeshika namba nne katika orodha za ubora duniani kuwa atashiriki michuano hiyo ya Brazil. Nadal ameshinda mataji 11 ya Grand Slams lakini maumivu yalipelekea nyota huyo raia wa Hispania kutocheza toka June mwaka jana. Nyota huyo alikosa michuano ya wazi ya Australia inayoendelea hivi kwa kupata maambukizi ya tumbo wakati akiendelea na matibabu ya mwisho ya mguu wake.

No comments:

Post a Comment