>>TATHMINI YA KUNDI kwa KUNDI!
Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013,
yanaanza huko Nchini Afrika Kusini Jumamosi Januari 19 kwa Mechi ya
ufunguzi ya Kundi A kati ya Wenyeji Afrika Kusini na Cape Verde kwenye
Uwanja wa Taifa Mjini Johannesburg.
IFUATAYO NI TATHMINI YA KILA KUNDI:
**FAHAMU: KILA KUNDI LITATOA TIMU 2 KUTINGA ROBO FAINALI.
KUNDI A:
-Afrika Kusini
-Cape Verde
-Morocco
-Angola
Wenyeji Afrika Kusini, wakishiriki
Fainali zao za 8, wametwaa Ubingwa wa Afrika mara moja tu pale Mwaka
1996 walipokuwa pia Wenyeji wa Fainali hizo ambako kwenye Fainali
yenyewe waliyotwaa Ubingwa waliichapa Tunisia Bao 2-0 Bao zote
zikifungwa na Mark Williams ambae aliwahi kuichezea Wolverhampton
Wanderers ya England.
Safari hii, Afrika Kusini, maarufu kama
Bafana Bafana, watacheza bila ya Staa wa Everton Stephen Pienaar ambae
alistaafu kuichezea Nchi yake Miezi mitatu iliyopita.
Katika Kundi hili, mpinzani mkubwa wa
Bafana Bafana anaonekana kuwa Morocco ambao walikuwa Washindi wa Pili wa
AFCON 2004 na ambao chini ya Kocha Rachid Taoussi wanaonekana kuimarika
huku Uwanjani wakiwategemea Maprofeshenali kadhaa wanaocheza Klabu
kubwa Ulaya wakiwemo Karim El Ahmadi wa Aston Villa, Beki wa Udinese
Mehdi Benatia na Mchezaji wa Fiorentina, Mounir El Hamadaoui.
Cape Verde, Timu changa inayoshiriki
Fainali zao za kwanza kwa kuwabwaga Vigogo Cameroun 3-2 kwenye mchujo,
wana Wachezaji kadhaa wanaocheza huko Ureno lakini tegemezi kubwa ni
Winga Ryan Mendes, Miaka 22, ambae alifunga Bao 3 kwenye Mechi za Mchujo
za AFCON 2013 na ambae aling’ara huko Ufaransa na Klabu ya Le Havre na kuzolewa na Klabu kubwa Lille Mwaka 2012.
Timu ya 4 ya Kundi A ni Angola ambao
mara mbili wametinga Robo Fainali za AFCON na kuishia hapo na mashine
yao ya Magoli ni Straika wa zamani wa Manchester United, Manucho, ambae
ana rekodi ya kufunga Bao 21 kwa Mechi 38 za Angola.
Manucho anazo Bao 6 kwa Klabu yake ya
sasa ya Spain, Real Valladolid, zikiwamo Bao 2 alizoipiga Real Madrid
walipokutana Mwezi uliopita.
KUNDI B:
-Ghana
-DR Congo
-Niger
-Mali
Bila shaka Ghana, moja ya Timu inayopewa nafasi kubwa kutwaa AFCON 2013,
ndio wanaopewa nafasi kubwa kuwa Nambari Wani kwenye Kundi hili na
wamesheheni Majina makubwa kama kina Asamoah Gyan, John Pantsil na John
Mensah lakini pia watawakosa Mastaa wengine, kina Michael Essien, Sulley
Muntari na Andre Ayew, ambao wamefyekwa toka Kikosini na Kocha James
Kwesi Appiah.
Mali na Congo DR ndizo zinazotegemewa
kuchuana ili kupata nafasi moja kuungana na Ghana kwenye Robo Fainali na
zote zina Mastaa maarufu huku Mali ikiwa nao Modibo Maiga wa West Ham
na Samba Diakite wa QPR lakini watamkosa Nahodha wao wa zamani Mahamadou
Diarra anaechezea Fulham kwa kuumia.
Hata hivyo, Mali wanae tena Mchezaji
Momo Sissoko, aliewahi kuichezea Liverpool na sasa yuko Juventus, baada
ya kutoichezea Mali kwa Miaka miwili.
Congo DR nao wana Mastaa wao lakini
atakaebeba jahazi ni Nahodha Tresor Mputu ambae aliwahi kufungiwa Miezi
12 wakati akiechezea Congo kwa kumpiga Refa.
Niger ni Timu ya 4 kwenye Kundi hili na
hii ni Fainali yao ya pili kucheza baada ya AFCON 2012 ambayo hawakuvuka
hatua ya Makundi na safari hii tena wanakadiriwa kufanya hivyo hivyo.
KUNDI C:
-Zambia
-Ethiopia
-Nigeria
-Burkina Faso
Kimaandishi, Nigeria wanaonekana kuwa
juu kwenye Kundi hili lakini ukweli ni kuwa Kundi hili liko wazi na
yeyote ana nafasi ya kusonga.
Nigeria wametinga Fainali za AFCON mara 6
lakini wamechukua Ubingwa mara mbili tu na baada ya kuzikosa AFCON 2012
Nchi hiyo ilimteua Mchezaji wao wa zamani, Stephen Keshi kuwa Kocha.
Keshi ameteua Kikosi mchanganyiko cha
Vijana wanaocheza Soka nyumbani na Maprofeshenali kama kina John Mikel
Obi na Victor Moses wa Chelsea na Beki wa zamani wa Everton, Joseph
Yobo.
Zambia ndio Mabingwa watetezi wa Afrika
baada ya kutwaa Taji la AFCON 2012 kwa kuichapa Timu kali Ivory Coast
kwa Mikwaju ya Penati 8-7 huko Nchini Gabon na pia wametinga Fainali
hizi za AFCON 2013 kwa Mikwaju ya Penati walipoitoa Uganda katika Mechi ya mwisho ya Mchujo.
Tegemezi la Zambia ni pamoja na Mchezaji
wa Southampton, Emmanuel Mayuka, Miaka 21, ambae ameichezea Klabu hiyo
ya England Mechi 8, 6 akitokea Benchi.
Timu nyingine za Kundi hili ni Ethiopia
na Burkina Faso lakini Ethiopia washawahi kuwa Mabingwa wa Afrika mara
moja walipotwaa Taji Mwaka 1962 na safari hii Penati ya Dakika ya mwisho
ya Mchezaji Adane Girma kwenye Mechi ya mwisho ya Mchujo na Benin ndio
imewaingiza Fainali za AFCON 2013.
Matokeo mazuri kwa Burkina Faso kwenye Mashindano haya ya Afrika ni kukamata nafasi ya 4 kwenye Fainali za Mwaka 1998.
KUNDI D
-Ivory Coast
-Togo
-Tunisia
-Algeria
Wanasema hili ndio ‘Kundi la Kifo!’
Lakini Timu ngumu Ivory Coast,
iliyosheheni Masupastaa wa kila aina, watataka kufanya vyema kupita
AFCON 2012 ambako walitolewa kwenye Fainali na Zambia kwa Matuta 8-7 na
safari hii kutwaa Ubingwa wa Afrika kwa mara ya Pili katika historia
yao.
Macho yote yatakuwa kwa Supa Straika
Didier Drogba, ambae licha ya mafanikio yake makubwa kwenye anga la
Soka, hajawahi kutwaa Ubingwa wa Afrika.
Togo wanatinga kwenye AFCON 2013 wakiwa
na habari njema baada ya Nahodha wao Emmanuel Adebayor kufuta msimamo
wa kususa kuichezea Nchi yake baada ya Rais wa Nchi hiyo kufanya
mazungumzo nae.
Wengine kwenye Kundi hili gumu ni
Algeria na Tunisia ambao kila mmoja ashawahi kuwa Bingwa wa Afrika mara
moja na Timu zote zina Wachezaji kadhaa ambao wako Ulaya.
Algeria wanatawategemea Kiungo wa
Valencia Sofiane Feghouli, Winga wa zamani wa Fulham na Watford, Hamed
Bouazza na Staa wa Nottingham Forest, Guedioura.
Nae Kocha wa Tunisia, Sami Trabelsi,
licha ya kuwa na Mastaa kadhaa, inaelekea amejitia kitanzi mwenyewe
baada ya kumtema Nyota Kiungo Nyota wa Atletico Madrid Kader Oueslati na
hili huenda likamfanya atimuliwe ikiwa hatafanikiwa kwani Tunisia,
ndani ya Miaka minne, washabadilisha Makocha mara 7.
RATIBA:
[SAA za BONGO]
Jumamosi Januari 19
South Africa v Cape Verde Islands [Soccer City Saa 1 Usiku]
Angola v Morocco [Soccer City Saa 4 Usiku]
Jumapili Januari 20
Ghana v Congo DR [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Mali v Niger Nelson [Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
Jumatatu Januari 21
Zambia v Ethiopia [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Nigeria v Burkina Faso [Mbombela Stadium Saa 3 Usiku]
Jumanne Januari 22
Ivory Coast v Togo [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Tunisia v Algeria [Royal Bafokeng Stadium Saa 3 Usiku]
Jumatano Januari 23
South Africa v Angola [Moses Mabhida Stadium Saa 12 Jioni]
Morocco v Cape Verde Islands [Moses Mabhida Stadium Saa 3 Usiku]
Alhamisi Januari 24
Ghana v Mali [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Niger v Congo DR [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
Ijumaa Januari 25
Zambia v Nigeria [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Burkina Faso v Ethiopia [Mbombela Stadium Saa 3 Usiku]
Jumamosi Januari 26
Ivory Coast v Tunisia [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Algeria v Togo [Royal Bafokeng Stadium Saa 3 Usiku]
Jumapili Januari 27
Morocco v South Africa [Moses Mabhida Stadium Saa 2 Usiku]
Cape Verde Islands v Angola [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 2 Usiku]
Jumatatu Januari 28
Congo DR v Mali [Moses Mabhida Stadium Saa 2 Usiku]
Niger v Ghana [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 2 Usiku]
Jumanne Januari 29
Ethiopia v Nigeria [Royal Bafokeng Stadium Saa 2 Usiku]
Burkina Faso v Zambia [Mbombela Stadium Saa 2 Usiku]
Jumatano Januari 30
Algeria v Ivory Coast [Royal Bafokeng Stadium Saa 2 Usiku]
Togo v Tunisia [Mbombela Stadium Saa 2 Usiku]
ROBO FAINALI
Jumamosi Februari 2
Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
Jumapili Februari 3
Mshindi Kundi D v Mshindi wa Pili Kundi C [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi Kundi C v Mshindi wa Pili Kundi D [Mbombela Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
NUSU FAINALI
Jumatano Februari 6
Mshindi RF 3 v Mshindi RF 2 [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi RF 1 v Mshindi RF 4 [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
MSHINDI wa TATU
Jumamosi Februari 9
[Nelson Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
FAINALI
Jumapili Februari 10
[Soccer City Saa 3 Usiku]
No comments:
Post a Comment