Friday, January 4, 2013

PRINCE-BOATENG AWATUMIA SALAMU ZA 2013 MASHABIKI WABAGUZI.


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ghana na klabu ya AC Milan, Kevin-Prince Boateng jana amewaongoza wachezaji wenzake kuondoka uwanjani kwa kususia mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya daraja la nne ya Pro Patria baada ya mashabiki kuwafanyia vitendo vya kibaguzi wachezaji weusi. Nyota huyo wa zamani wa klabu ya Tottenham Hotspurs na Portsmouth alikamata mpira na kuupiga kuelekea kwa mashabiki waliofanya vitendo hivyo katika dakika ya 26 ya mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Busto Arsizio kilometa 20 kaskazini-magharibi mwa jiji la Milan. Mchezo huo ulisitishwa baada ya wachezaji wote wa Milan kuungana na Boateng kwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo huku wachezaji wa Pro Patria wakijaribu kuwabembeleza ili warejee kuendelea na mchezo huo. Wachezaji weusi waliolengwa kufanyiwa vitendo hivyo kwenye mchezo huo mbali na Boateng ni pamoja na M’Baye Niang, Urby Emanuelson na kiungo wa zamani wa Portsmouth Sulley Muntari ambapo juhudi za mshehereshaji wa mchezo huo kujaribu kuwakanya mashabiki hao zilishindikana.

No comments:

Post a Comment