Friday, January 4, 2013

YANGA KIBARUANI KESHO UTURUKI.


Timu ya Yanga kesho itashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na tim ua Arminia Bielefeld ya Ujerumani katika mchezo utakaofanyika mjini Antalya majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki na Kati. Young Africans ambayo imeweka kambi ya mafunzo katika mji wa Antalya imekuwa ikifanya mazoezi tangu siku ya jumatatu na wachezaji wote wameonekana kufurahia mazingira ya kambi na huduma zote kwa ujumla. Baada ya kufanya mazoezi kwa takribani siku tano (5) mfiululizo itatumia mchezo wa kesho dhidi ya timu ya Arminia Bielefed kama kipimo tosha cha maendeleo ya mafunzo yanayoendelea nchini Uuturuki. Kocha Mkuu wa Young Africans mholanzi Ernie Brandts amesema anashukuruika wachezaji wake wapo fit kwa ajili ya mchezo kesho, na kwa kuwa hakuna mchezaji majeruhi atakuwa na fursa ya kumtumi amchezaji yoyote katika mechi hiyo. Aidha Brandst amesema kuwa anajua mchezo wa kesho utakua mgumu kwani timu ya Arminia Bielefeld ni timu nzuri na imekua ikishiriki ligi kuu ya ujerumani mara kadhaa, hivyo ni timu ambayo itatoa ushindani mkubwa sana

No comments:

Post a Comment