Friday, January 4, 2013

AYEW HATIHATI KUSHIRIKI AFCON.


KLABU ya Olympique Marseille ya Ufaransa imesema kuwa mshambuliaji wake nyota Andre Ayew ameumia goti wakati wa mazoezi Januari 2 ambapo waliliandikia Shirikisho la Soka la Ghana-GFA juu ya taarifa hizo. Habari za kuumia kwa Ayew zitakuwa ni pigo lingine kwa kocha wa timu ya taifa ya Ghana baada ya mshambuliaji wake mwingine kati ya wanne aliowateua kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon Yahaya Mohammed naye kuwa majeruhi. GFA nayo imewaagiza Marseille kumuachia Ayew kwenda jijini Abu Dhabi ili waweze kumfanyia uchunguzi wenyewe kama ataweza kushiriki michuano ya Afcon ambayo itafanyika nchini Afrika Kusini kuanzia Januari 19 mwaka huu. Ghana kwasasa ipo UAE kwa ajili ya michezo ya kirafiki dhidi ya Misri na Tunisia kabla ya kuelekea nchini Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment