Friday, January 4, 2013

ULIKUWA UAMUZI RAHISI KUHAMIA CHELSEA - BA.


MSHAMBULIAJI mpya wa klabu ya Chelsea, Demba Ba amesisitiza kuwa ulikuwa ni uamuzi rahisi kusaini mkataba na mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya uhamisho wake kuthibishwa na klabu hiyo mapema leo. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal amesaini mkataba wa miaka mitatu na nusu akitokea klabu ya Newcastle kwa uhamisho wa paundi milioni 7.5. 
Ba mwenye umri wa miaka 27 ambaye atakuwepo katika benchi la wachezaji wa akiba kwa ajili ya mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Southampton kesho atakuwa anavaa fulana yenye namba 29. Akihojiwa nyota huyo amesema uamuzi wa kujiunga na Chelsea ulikuwa rahisi kwake haswa ikizingatiwa kuwa timu hiyo ndio mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

No comments:

Post a Comment