Friday, January 4, 2013

AZARENKA AMKWEPA SERENA WILLIAMS


MCHEZA tenisi nyota anayeshika namba moja katika orodha za ubora wa mchezo duniani kwa upande wa wanawake, Victoria Azarenka amejitoa katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya kimataifa ya Brisbane ambapo alikuwa apambane na Serena Williams. Zikiwa zimebakia dakika 30 kabla ya mchezo wake na Williams wa Marekani kuanza, Azarenka ambaye ni bingwa mtetezi wa michuano ya wazi ya Australia alitangaza kujitoa baada kuumia kidole gumba katika mkono wake wa kulia. Azarenka mwenye umri wa miaka 23 raia wa Belarus amesema amekuwa na maumivu hayo kwa kipindi cha siku kumi na yamekuwa yakiongezeka ndio maana ameamua kujitoa ili apate muda wa kujitibu kabla ya kuanza kwa michuano ya Australia. Nyota huyo amesema kulikuwa na kucha ambayo ilikuwa ikimsumbua katika kidole chake gumba lakini kadri siku zilivyokuwa zikisonga mbele tatizo hilo lilizidi na kumnyima raha ya kucheza kwa kiwango chake.

No comments:

Post a Comment