Tuesday, January 15, 2013

KADI NYEKUNDU ya KOMPANY YAFUTWA NI JINSI GANI MAREFARII BADO HALI TETE HATA ULAYA!!

>>MAN CITY WASHINDA RUFAA!!
JOEY_BARTON_n_KOMPANYNAHODHA wa Mabingwa wa England Manchester City, Vincent Kompany, leo amepona Kifungo cha Mechi 3 baada ya Kadi Nyekundu aliyopewa na Refa Mike Dean juzi Jumapili, Man City walipoichapa Arsenal 2-0 kufutwa na Tume Huru ya FA, Chama cha Soka England, kufuatia Rufaa iliyowasilishwa na Klabu yake.
Kompany alipewa Kadi Nyekundu katika Kipindi cha Pili, Dakika ya 75, alipokuwa akimkabili Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere.
Mara baada ya Mechi hiyo, Meneja wa Man City Roberto Mancini alidai kutolewa kwa Kompany ni kosa kubwa la Refa Mike Dean.
Endapo kama Kadi hiyo ingebaki kama ilivyo, Kompany angezikosa Mechi 3 dhidi ya Fulham na QPR, kwenye Ligi Kuu England, na Mechi ya Raundi ya 4 ya FA CUP dhidi ya Crystal Palace au Stoke City.
Katika Mechi hiyo hiyo ya Arsenal na Man City, Beki wa Arsenal, Laurent Koscielny, alitolewa nje katika Dakika ya 10 tu kwa kumshika Edin Dzeko, kosa ambalo pia lilizaa Penati iliyopigwa na Edin Dzeko lakini Kipa Szczesny aliokoa baada ya mpira kupiga posti.
Arsenal hawakukata Rufaa kupinga adhabu hiyo

No comments:

Post a Comment