Sunday, February 3, 2013

UKURASA WA HABARI ZA KIMATAIFA: Wenger akunwa na mwanzo mzuri wa Nacho Monreal. Dembele awaonya wenzake kukosa nafasi nne za juu mwisho wa msimu na Michael Owen kukumbana na adhabu ya FA.




Bosi wa Arsenal Arsene Wenger amefurahishwa na kiwango cha soka kilionyeshwa na nyota wake mpya Nacho Monreal katika mchezo ambao washika bunduki waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stoke hapo jana.
Katika mchezo huo Lukas Podolski alifunga goli pekee kunako dakika ya 78 ambalo limeifanya Arsenal kujikita katika nafasi ya 4 ya msimamo wa ligi huku Monreal akiwaonyesha jitihada kubwa katika sehemu ya ulinzi kwa mara ya kwanza.
Mlinzi huyo mpya alikuwa na muda mdogo sana wa kuzoea kikosi chake kipya akihitaji kijigeuza kidogo tu na kufanana na aina ya uchezaji wa timu hiyo yenye maskani yake Emirates kabla ya kuingia katika kikosi cha kwanza ambapo Wenger anaamini ulikuwa ni usajili chanya kumpata mhispania huyo.
Amekaririwa akisema kuwa pengine ingekuwa ni ngumu kwake kwani alikuwa anakutana na timu inayotumia nguvu sana nay eye akitokea katika soka la Hispania lakini anadhani Monreal ameweza.
"Jambo linalo ridhisha ni kwamba Monreal amekuwa na mwanzo mzuri, kwa mchezaji kuwasili jana na leo kuwa katika timu kwa ujumla alikuwa akiimarika kadri mchezo ulivyokuwa unaendelea"
Dembele akatishwa tamaa na kupata nafasi 4 za juu za msimu huu.
 Kiungo wa Tottenham Moussa Dembele amewaonya wachezaji wenzake kwamba wako katika hatari ya kuwa nje ya nafasi nne za juu katika ligi kuu ya soka nchini England, na kusema labda wabadilike na kurudi katika njia ya kusaka ushindi katika michezo inayoendelea ya ligi hiyo.
Amenukuliwa akisema
"Ukiangalia timu tuliyonayo hatuna sababu ya kuogopa timu yoyote katika Premier League, lakini tunakosa nafasi nyingi za kufunga, wakati mwingine tunapoteza points katika mchezo ambao tulistahili kushinda, inachanganya sana. Tuliposhinda Old Trafford msimu uliopita tulicheza mchezo mzuri sana.
Angalia sasa Arsenal, Chelsea, Liverpool wanapoteza points tulipaswa kuwa mbele yao”
Michael Owen kukabiliwa na adhabu ya FA
 Mshambuliaji wa Stoke Michael Owen huenda akakumbana na adhabu ya chama cha soka nchini England FA baada ya kuonekana akimfanyia kitendo kisichokuwa cha kiungwana kiungo wa Arsenal Mikel Arteta.
Wawili hao walikumbana katika harakati za kuwania mpira dakika za lala salama katika mchezo uliomalizika kwa Arsena kuibuka na ushindi wa bao 1-0 hapo jana, ambapo Arteta alikwenda kumkabili Owen ambaye alimsukuma kwa nyuma.
Mwamuzi Chris Foy hakutoa adhabu kwa ya kadi kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33 lakini kamera ilimuonyesha Owen akifanya kitendo hicho.
Hata hivyo bosi wa Stoke Tony Pulis baadaye akikaririwa akisema
"Arteta ndiye aliyemkabili ndivyo sivyo Owen na kwamba Michael hakufanya hivyo”

No comments:

Post a Comment