Tuesday, January 15, 2013

BPL: MECHI PEKEE LEO, KIPORO CHELSEA v SOUTHAMPTON!

BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
Jumatano Januari 16
[SAA 4 DAK 45 Usiku]
Chelsea v Southampton

MABINGWA wa ULAYA, Chelsea, leo Usiku watakuwa kwao Stamford Bridge kucheza Mechi yao ya Kiporo cha BPL, Barclays Premier League, dhidi ya Southampton.
Mechi hii ilikuwa ichezwe Mwezi Desemba lakini iliahirishwa kwa vile Chelsea walisafiri kwenda kwenye Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani huko Japan.
Wakiwa nafasi ya 3 kwenye Ligi, Pointi 7 nyuma ya Man City na Pointi 14 nyuma ya Vinara Man United, Chelsea wana umuhimu wa kushinda Mechi dhidi ya Southampton ambao wako nafasi ya 15 na wana Pointi 21, ili wao wapunguze pengo dhidi ya Klabu za Jiji la Manchester.
Katika Mechi 6 zilizopita za Ligi, Chelsea wameshinda Mechi 5.

MSIMAMO-Timu za Juu:
1 Man United Mechi 22 [Tofauti ya Magoli 27] Pointi 55
2 Man City Mechi 22 [Tofauti ya Magoli 24] Pointi  48
3 Chelsea Mechi 21 [Tofauti ya Magoli 24] Pointi 41
4 Tottenham Mechi 22 [Tofauti ya Magoli 22] Pointi 40
5 Everton Mechi 22 [Tofauti ya Magoli 22] Pointi 37
6 Arsenal Mechi 21 [Tofauti ya Magoli 16] Pointi 34
7 West Brom Mechi 22 [Tofauti ya Magoli 1] Pointi 33
8 Liverpool Mechi 22  Tofauti ya Magoli 7] Pointi 31
9 Swansea Mechi 22 [Tofauti ya Magoli 5] Pointi 30
10 Stoke Mechi 22 [Tofauti ya Magoli -3] Pointi 29

Baada ya kuwa na wasiwasi wa kuwakosa Mastraika wao Demba Ba na Fernando Torres ambao walikuwa wakisumbuliwa na maumivu ya paja kwa Ba na ugonjwa kwa Torres, Chelsea wamethibitisha Wachezaji hao wote wako fiti.

MECHI NYINGINE LEO USIKU:
FA CUP-Raundi ya 3=MARUDIANO
Jumatano Januari 16
[SAA 4 Dak 30 Usiku]
Arsenal v Swansea City
[SAA 5 Usiku]
Man Utd v West Ham

DEMBA_BA-ATUA_CHELSEALakini, upo uwezekano wa Chelsea kutomuanzisha Nahodha wao John Terry ambae amepona Goti lakini bado anakosa pumzi kwa Mechi.
Pia Chelsea itawakosa Wachezaji wawili kutoka Nigeria, John Obi Mikel na Victor Moses, ambao wako na Timu ya Taifa kwa ajili ya AFCON 2013 inayoanza Jumamosi hii.
Kwa upande wa Southampton, Wachezaji watakaokosekana ni Chipukizi wa Miaka 17 Luke Shaw, Jose Fonte na Nahodha wao Adam Lallana wote wakiwa na maumivu.
USO kwa USO:
-Chelsea wameshinda Mechi 5 za mwisho walizocheza na Southampton na kufunga Jumla ya Bao 15.
-Mara ya mwisho Southampton kushinda Stamford Bridge ilikuwa Bao 4-2 Mwaka mpya 2002 huku Straika wao hatari wakati huo, James Beattie, akipiga Bao 2.

BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA:
Jumamosi Januari 19
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Norwich
Man City v Fulham
Newcastle v Reading
Swansea v Stoke
West Ham v QPR
Wigan v Sunderland
[SAA 2 na Nusu Usiku]
West Brom v Aston Villa
Jumapili Januari 20
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Chelsea v Arsenal
[SAA 1 Usiku]
Tottenham v Man United

No comments:

Post a Comment