Tuesday, January 15, 2013

DIDAS KUNDE AJITAPA KUWAKANDAMIZA RHINO RANGERS HII LEO KATIKA DIMBA LA ALLY HASSAN MWINYI


 
Kocha msaidizi wa timu ya kombaini wilaya ya Tabora mjini bw.Didas Kunde amesema leo piga uwa garagaza muhimu awafunge wapiga kwata wanajeshi wa hapa mkoani tabora na ambao wapo ligi daraja la kwanaza RHINO RANGERS katika mchezo wa kirafiki utakaocheza katika dimba la ALLY HASSAN MWINYI.
M,chezo huo utakuwa wa marudiano kutokana na mchezo wa awali juzi timu ya RHINO RANGERS iliweza kuibuka na ushindi wa bao 2-0 mabao yaliyofungwa na shija sanju na maghembe kipindi cha kwanza kutokana na uzembe wa mabeki wa timu ya kombaini wilaya.

Kwa upande wa timu ya RHINO RANGERS BW.Shija amesema leo wanatarajia kupanga kikosi cha cha kwanza ambacho kitakuw akipimo kizuri kw atimu ya Kagera Sugar ambayo inatarajia kuja kesho au kesho kutwa kuja kucheza na maafande hawa wa tabora kuelekea katika mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza FDL.

Kikosi cha kombaini wilaya kinaundwa na Mrisho Khalfan,Jackson Sebene,John Zacharia,Josephat  Miggi,Godfrey Magaso,Nassoro Mfoi,Khamis Bingwa,Binamungu Shabaan,Maiko Maningu,Zamoyoni Maiko na Abdalah Juma.

Wengine ni Kilanga Faraji,Mwinyira Stanley,Rashid Kopa,mMsafiri Peter,Herison Moses na Songoro Kasongo wakati makocha ni ANDREW ZOMA Kocha mkuu akisaidiwa na DIDAS KUNDE Kocha msaidizi.
 WAKATI HUO HUO Kuelekea mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza rhino rangers imeendelea kuimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji watano ili kuongeza nguvu katika kikosi,wachezaji iliowasajili ni ayoub iddy ,na josephy mapunda nafasi ya beki,doi mobby,mganda mchembe washambuliaji,na emanuely noely nafasi ya kiungo.

wachezaji wa zamani ni abdukarim mtumwa,iddy kihulya,charles mpinuki,james mwambembe,julius masunga,abass mohamedy,stanslaus mwakitosi,steven madhanda,shija sanju,shija mongo,salum mamro,salum majid,usi makame,na frank koe. 

wengine ni josephy salaganda,victor hangaya,bakary mahadhi,said kipanga,issa mohamedy,stanley mlai,samwely mwamasangula,omary magesa,msafiri maiko,ramadhani shabyeji na ally rumba na kuhitimisha idadi ya wachezaji 30 katika klabu hiyo inayonolewa na kocha wa zaman wa mafunzo ya zanzibar akisaidiwa na kocha mongo.

No comments:

Post a Comment