Tuesday, January 15, 2013

GORDON STRACHAN MENEJA MPYA SCOTLAND

GORDON_STRACHAN
>>STRACHAN ADAI: 'FALSAFA YANGU NI KUSHINDA KAMA MAN UNITED!'
Chama cha Soka cha Scotland, SFA, kimethibitisha uteuzi wa Gordon Strachan kama Meneja mpya wa Timu ya Taifa ya Scotland.
Strachan, mwenye Miaka 55, amekuwa hana kibarua tangu atoke Klabu ya Middlesbrough Oktoba 2010 lakini sasa amepewa kuiongoza Nchi ya Utaifa wake hadi baada ya EURO 2016.
Akipokea uteuzi huu, Strachan alisema: "Kila Klabu unayokwenda zipo changamoto, na sasa ni mara ya kwanza changamoto zipo mbele ya Taifa. Ukifanikiwa utalifanya Taifa lote liwe na furaha na kujisikia fahari na hicho ni kipaumbele kwangu kuweza kufanya hivyo kwa kusaidiwa na Watu wengine."

Gordon Strachan
-Alianza kucheza Soka Klabu ya Dundee huko Scotland kabla kujiunga Aberdeen Mwaka 1977.
-Alitwaa Ubingwa mara mbili, Scotland Cup mara 3, Kombe la Washindi Ulaya na European Super Cup akiwa na Aberdeen.
-1984 alijiunga na Manchester United na kutwaa FA Cup Mwaka 1985.
-Alidumu Leeds United Miaka 6 na kuiwezesha kupanda Daraja na kutwaa Ubingwa Daraja la juu.
-Ang’atuka Uchezaji akiwa na Coventry na kuingia Umeneja ambako alikaa Miaka mitano.
-Alifika Fainali ya FA CUP akiwa Bosi wa Southampton ambako alikaa Miaka mitatu.
-Mwaka 2005 ajiunga na Celtic kama Meneja na kutwaa Ubingwa mara 3 na kuifikisha Raundi ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI mara mbili.
-Mwaka 2009 awa Meneja wa Middlesbrough na kukaa Mwaka mmoja.

Akizungumzia malengo yake na Scotland, Strachan amesema anataka kuipeleka Nchi hiyo Fainali za Kombe la Dunia na EURO, kibarua ambacho ni kigumu hasa kwa vile mara ya mwisho kwa Scotland kufika Fainali za Mashindano makubwa ilikuwa ni Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 1998 zilizochezwa huko France.

KOMBE LA DUNIA-BRAZIL 2014
[MCHUJO KANDA YA ULAYA]
MSIMAMO
KUNDI A
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Belgium Pointi 10
2 Croatia 10
3 Serbia 4
4 Macedonia 4
5 Wales 3
6 Scotland 2

Hadi sasa kwenye Kundi lao la Mechi za Mchujo kuwania kwenda Brazil Mwaka 2014 kwenye Fainali za Kombe la Dunia, Scotland imevuna Pointi 2 tu lakini hilo halikumkatisha tamaa Gordon Strachan ambae ametamka: “Kama tukifanya kazi pamoja kwa umoja najua fika tutafanikiwa. Falsafa yangu ni kushinda Gemu za Soka kama Manchester United!”
Mechi ya kwanza ya Strachan kwenye himaya yake kama Meneja wa Scotland ni ile ya Kirafiki dhidi ya Estonia Mwezi ujao Februari 6.

No comments:

Post a Comment