OBI MIKEL AJINYAKULIA KITITA CHA DOLA 5,000 KUTOKA KWA KALOU.
KIUNGO wa kimataifa wa
Nigeria John Obi Mikel amejinyakulia cha dola 5,000 kutoka kwa mchezaji
mwenzake wa zamani wa Chelsea Salomon Kalou baada ya Nigeria kuiengua
Ivory Coast katika michuano ya Mataifa ya Afrika jijini Rustenburg,
Afrika Kusini. Nigeria
ambao wanajulikana kama Super Eagles walifanikiwa kuwatoa Tembo wa
Ivory Coast ambao walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kunyakuwa taji la
michuano hiyo kwa mabao 2-1. Kabla
ya mchezo huyo Obi Mikel na Kalou waliekeana dau kila mmoja akidai timu
yake itasonga mbele kwenye michuano hiyo lakini ilikuwa ni Kalou ambaye
anacheza katika klabu ya Lille ya Ufaransa aliyelazimika kutimiza ahadi
yake baada ya timu yake kutolewa. Akihojiwa
Kalou mwenye umri wa miaka 27 aliwasifu wapinzani wao kwa kucheza
mchezo mzuri na kwamba walistahili kushinda mchezo huo huku akidai kuwa
ametimiza ahadi yake aliyompa Obi Mikel. Kwa
upande mwingine Obi Mikel amesema juhudi za pamoja walizokuwanazo
kwenye mchezo huo ndio siri ya ushindi wao waliopata dhidi ya timu hiyo
ngumu. Nigeria
sasa itakwaana na Mali katika mchezo wa nusu fainali itakayofanyika
katika Uwanja wa Moses Mabhida uliopo jijini Durban Jumatano.
No comments:
Post a Comment