Saturday, January 12, 2013

AFCON 2013: WIKI MOJA IMEBAKI!!


AFCON_2013_LOGOIKIWA imebaki Wiki moja tu kwa Mashindano ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, kuanza huko Afrika Kusini kwa Mechi ya ufunguzi ya Kundi A kati ya Wenyeji Afrika Kusini na Cape Verde itayochezwa Januari 19 huko Johannesburg, Kamati ya Maandalizi imesema Mauzo ya Tiketi imefikia 320,000 kati ya Tiketi 500,000 zilizotolewa kuuzwa.
Kamati ya Maandalizi imesema kudorora kwa Mauzo ya Tiketi hizo kunatokana na upungufu katika mikakati ya mauzo.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
AFCON 2013
MAKUNDI:
KUNDI A: South Africa, Cape Verde, Morocco, Angola
KUNDI B: Ghana, DR Congo, Niger, Mali
KUNDI C: Zambia, Ethiopia, Nigeria, Burkina Faso
KUNDI D: Ivory Coast, Togo, Tunisia, Algeria
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Wakati huo huo, Marefa 18 na Marefa Wasaidizi 21 ndio wameteuliwa kuchezesha Mechi za AFCON 2013 na kati yao Marefa wawili na Wasaidizi 8 ndio wapya kutoka wale waliochezesha AFCON 2012 huko Equatorial Guinea na Gabon Mwezi Januari 2012.
Huku Nigeria ikiwa haikutoa hata Mwamuzi mmoja, Marefa wapya ni Sylvester Kirwa wa Kenya na kutoka Seychelles  ni Bernard Camille na Wenyeji Afrika Kusini wametoa Marefa wawili, Daniel Bennett na Zakhele Siwela.
Algeria na Senegal ndio zenye Waamuzi wengi huku kila mmoja ikitoa Marefa watatu.
Marefa hao wanatarajiwa kujumuika Januari 15 Mjini Johannesburg kwa kufanyiwa Vipimo na Majaribio ya mwisho.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
AFCON 2013==AFRIKA KUSINI
VIWANJA:
-Soccer City, Johannesburg [Mashabiki 94,700]
-Moses Mabhida Stadium, Durban [Mashabiki 54,000]
-Nelson Mandela Bay Stadium, Port Elizabeth [Mashabiki 48,000]
-Mbombela Stadium, Nelspruit [Mashabiki 41,000]
-Royal Bafokeng Stadium, Rustenburg [Mashabiki 42,000]
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi Januari 19
South Africa v Cape Verde Islands [Soccer City Saa 1 Usiku]
Angola v Morocco [Soccer City Saa 4 Usiku]

No comments:

Post a Comment