Saturday, January 12, 2013

MOROCCO YAMTAKA TAARABT KUOMBA RADHI.


SHIRIKISHO la Soka nchini Morocco limemtaka kiungo wa kimataifa wa nchi hiyo Adel Taarabt kuomba radhi kufuatia kumkashifu kocha wa timu ya taifa Rachid Taoussi ambaye alimuacha katika kikosi kitakachoshiriki michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon. Kiungo huyo anayecheza katika klabu ya Queens Park Rangers ya Uingereza anatuhumiwa kumtumia ujumbe wa kumdhalilisha Taoussi na vyombo vya habari vya nchi hiyo kufuatia kuenguliwa katika michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika nchini Afrika Kusini. Katika taarifa yake iliyotolewa katika vyombo vya habari, shirikisho linamtaka mchezaji huyo kuomba radhi kwa maandishi kufuatia maneno yake ya kashfa aliyotoa. Taoussi alimuacha Taarabt mwezi uliopita akidai kuwa nyota huyo alikataa kuonana naye wakati akifanya ziara barani Ulaya Octoba mwaka jana kwa ajili ya kuangalia wachezaji atakaowatumia katika Afcon.

No comments:

Post a Comment