Thursday, January 10, 2013

BAADA YA JANA MNYAMA KUSHINDWA KUUNGURUMA VISIWANI LEO NI TUSKER NA MIEMBENI KATIKA UWANJA WA AMAAN NUSU FAINALI YA PILI


Monja Liseki wa Miembeni
TUSKER FC inashuka dimbani leo usiku kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar kumenyana na Miembeni katika Nusu Fainali ya pili ya Kombe la Mapinduzi.
Mchezo huo, unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua, kwani kwa sasa Miembeni ndiyo timu inayoiwakilisha vema Zanzibar katika mashindano haya na inaungwa mkono na Wazanzibari wengi.
Kocha wa Miembeni Salum Bausi amesema hawahofii Tusker na leo atawaonyesha kwamba mpira ni zaidi yua nguvu 
Nahodha wa Tusker, Joseph Shikokoti amesema kwamba haoni timu ya kuwazuia kutwaa Kombe la Mapinduzi.
Shikokoti aliyewahi kuchezea Yanga alisema kwamba anafahamu Azam ni wazuri na  watakutana nayo fainali, lakini hawawezi kuwazuia wasitwae Kombe.
“Hili Kombe letu, tumeona uwezo wa Azam ni wazuri, lakini tutawafunga tukikutana nao, hawana uwezo wa kutuzuia,”alisema Shikokoti.
Katika Nusu Fainali ya kwanza jana,Azam iliitoa Simba SC kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120

No comments:

Post a Comment