Thursday, January 10, 2013

MUACHENI MOURINHO AFANYE KAZI YAKE - RONALDO.


MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuacha kumshambulia Jose Mourinho na badala waelekeze nguvu zao katika kuiwaunga mkono. Kauli hiyo ya Ronaldo imekuja kufuatia mashabiki wa klabu hiyo kumzomea Mourinho kabla ya kuanza kwa mchezo Kombe la Mfalme dhidi ya Celta Vigo ambao ulichezwa katika Uwanja wa Santiago Bernabeu huku Madrid walishinda mchezo huo kwa mabao 4-0. Katika mchezo huo Ronaldo ambaye ndiye mfungaji anayeongoza katika klabu hiyo akiwa amepachika mabao 174 katika michezo 172 aliyocheza toka ahamie kutoka Manchester United alifunga mabao matatu na na kuibuka nyota wa mchezo huo. Ronaldo amesema mashabiki hao inabidi waache tabia hiyo kwani bado kuna mataji mengi ambayo wanaweza kushinda mwaka huu na akiwa kama kocha lazima awe na uamuzi wa mwisho hivyo mashabiki na wachezaji wanapaswa kuheshimu na kumuunga mkono.
No comments:

No comments:

Post a Comment