Thursday, January 10, 2013

RONALDO APIGA HAT-TRICK AKIISAIDIA REAL MADRID KUTINGA ROBO FAINALI YA KING'S CUP AU COPA DEL REY NA HUKO ITALY KIBIBI CHAONYESHA UMWAMBA KWA AC MILAN .


MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ureno na klau ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo jana amekuwa nyota ya mchezo baada ya kufanikiwa kuifungia klabu yake mabao matatu katika ushindi wa mabao 4-0 waliopata dhidi ya Celta Vigo ambao umewapeleka katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Mfalme. Ronaldo ambaye alishika nafasi ya pili katika tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa dunia, alifunga mabao mawili ndani ya dakika 25 za kipindi cha kwanza na kumalizia lingine moja katika dakika za lala salama na kuihakikishia timu yake ushindi. Madrid imefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuifunga Celta Vigo kwa jumla ya mabao 5-2 kwenye michezo miwili waliyokutana na sasa wanatarajia kukutana na Valencia wiki ijayo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo alisifu uwezo wa nyota huyo ambao umekuwa ukiisaidia klabu hiyo kupata matokeo mazuri.

COPA del REY
MATOKEO/RATIBA-MECHI za MARUDIANO
[Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili katika Mabano]
Jumatano Januari 9
Sevilla 1 Real Mallorca 2 [6-2]
Real Madrid 4 Celta Vigo 0 [5-2]
Real Zaragoza 2 Levante 0 [3-0]
Alhamisi Januari 10
Getafe v Atletico Madrid [0-3]
Barcelona v Cordoba [2-0]
Real Betis v Las Palmas [1-1]

COPPA ITALIA

ROBO FAINALI
RATIBA/MATOKEO:
Jumatano Januari 9
Juventus 2 AC Milan 1
Jumanne Januari 15
Inter Milan v Bologna
Jumatano Januari 16
Fiorentina v AS Roma

Vucinic aifikisha Juve Nusu Fainali
Bao la Dakika za nyongeza la Mirko Vucinic limewafikisha Mabingwa Italy, Juventus, Nusu Fainali ya COPPA ITALIA walipotoka nyuma kwa Bao moja na kuifunga AC Milan Bao 2-1.
AC Milan, ambao pia Msimu uliopita walitupwa nje na Juve katika hatua kama hii, waliongoza kwa Bao la Dakika ya 6 la Stephan El Shaarawy lakini Juventus walisawazisha kwa frikiki ya Sebastian Giovinco.
Hadi Dakika 90 zinakwisha Bao zilikuwa 1-1 na ndipo Dakika 30 za Nyongeza zikachezwa na katika Dakika ya 6 tu ya muda huo, Mirko Vucinic akafunga Bao la ushindi kwa Juventus ambao sasa watacheza na Lazio kwenye Nusu Fainali.

No comments:

Post a Comment